Friday 8 May 2015

Pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara 2014-15 lafungwa Jumamosi



Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga.

Na Mwandishi Wetu
TIMU 14 ZA Ligi Kuu Tanzania Bara leo zinashuka kwenye viwanja tofauti viwanja tofauti kumaliza mechi zao za mwisho za kumalizia msimu wa 2014/2015.

Leo ndio itajulikana wazi timu zipi mbili zitakazoshuka daraja baada ya bingwa na mshindi wa pili tayari kujulikana katika kinyanganyiro hicho kilichoanza mwaka jana.

Yanga ndio mabingwa wapya wakati waliokuwa mabingwa Azam FC wameshika nafasi ya pili huku Polisi Morogoro ndio iko kwenye hatari zaidi ya kushuka daraja baada ya kushika mkia katika msimamo wa ligi hiyo yenye timu 14.

Washindi wa Pili Tanzania Bara.
Polisi wenye pointi 25 wanakabiliwa na kibarua kizito dhidi ya Mbeya City, mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Tayari Mbeya City yenye pointi 31 ilishajiondoa kwenye mstari mwekundu wa kushuka, hivyo itakuwa ni kazi kwa timu hiyo ya Morogoro. Iwapoitashinda itafikisha pointi 28, ambazo haziwezi kumvusha popote.

Lakini kama wataruhusu kufungwa pia bado ni lazima washuke daraja. Maafande hao ambao wamekuwa wakishuka na kupanda kila baada ya miaka kadhaa, wameshacheza michezo 25, wameshinda mitano, sare 10 na kupoteza 10.

Timu zinazofuatana nane zikiwamo Stand United, Mgambo Shooting, Ndanda FC na Tanzania Prisons nazo ziko hatarini kama zitashindwa kufanya vizuri katika michezo ya leo kwa vile hufungana kwa pointi sawa 28.

Stand United inaikaribisha Ruvu Shooting yenye pointi 29 kwenye Uwanja wa Kambarage Shinyanga.

Timu hizi mbili zimetofautiana kwa pointi moja, ambazo kama hazitashinda, moja itakuwa hatarini ikiwa nyingine zitashinda.

Stand United wameshacheza michezo 25, wameshinda saba, wana sare saba, wamepoteza michezo 11, hivyo wanahitaji kushinda leo ili kuendelea kubaki kwa msimu mwingine hasa ikizingatiwa wamepanda kwa mara ya kwanza msimu huu.

Mgambo Shooting inamaliza na Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex, Timu hii yenye maskani yake Tanga ina uwezekano wa kushuka kama haitashinda mchezo huo mgumu kwao. 

Simba kutopanda ndege tena baada ya kushika nafasi ya tatu msimu huu.
Tayari wameshacheza michezo 25, wameshinda nane, sare nne na wakifanya mzaha watashuka na kuwapa nafasi African Sports iliyopanda daraja ya kuchukua nafasi yake.

Kwa upande wa Ndanda FC inamaliza mchezo wake na Yanga utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Timu nyingine ni Tanzania Prisons, ambayo inacheza dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Maafande hao wanahitaji kushinda ili kuendelea kubaki na pia Kagera wanahitaji ushindi.

Michezo mingine ni kati ya Simba itakayokwaruzana na JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, huku Coastal Union ikicheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu.

Timu tano zinazofungana kwa pointi 31 ni Coastal Union, JKT Ruvu, Mtibwa Sugar, Mbeya City na Kagera Sugar.

Zote zinahitaji ushindi kujitofautisha na zile ambazo zina pointi 28 ambazo zikishinda zinaweza kufanana na wao.

 Msimamo:




MPWDLGFGA+/-Pts

1
Young Africans25174452173555

2
Azam25139336181848

3
Simba SC25128536181844

4
Mtibwa Sugar2571082424031

5
Mbeya City2571082122-131

6
Kagera Sugar2587102226-431

7
JKT Ruvu2587101923-431

8
Coastal Union2571081924-531

9
Ruvu Shooting2578101628-1229

10
Tanzania Prisons2551371822-428

11
Ndanda2577112029-928

12
Mgambo JKT2584131828-1028

13
Stand United2577112234-1228

14
Polisi Morogoro25510101626-1025

No comments:

Post a Comment