Tuesday, 5 May 2015

Maoni ya makocha, viongozi kuhusu makundi Ligi ya Mabingwa AfrikaCAIRO, Misri
BAADA ya kupangwa kwa makundi ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika leo Jumanne, yafuatayo ni maoni ya viongozi na makocha wa timu zinazoshiriki hatua hiyo wakizungumza ratiba hiyo.

Hatem Abdel Gaafar (Timu Meneja, El Merreikh)
Ratiba ni nzuri na tunatarajia kufanya vizuri. Hii ni mara yetu ya pili kucheza hatua hii ya makundi. Lengo letu ni kutwaa ubingwa na hilo tutalifanyia kazi.

Wael Gomaa (Mkurugenzi wa Soka, Al Ahly)
Tulitarajia kupangwa dhidi ya timu ngumu, kutokana na ushiriki wa klabu zenyewe tangu mwanzo. Karibu klabu 10 angalau zimewahi kutwaa moja ya mataji ya Afrika huko nyuma.

Hivyo tulijua itakuwa ngumu kwetu kutetea taji tuliloshinda mwaka jana. Tuna wachezaji wazuri na kocha (Fathi Mabrouk) ambaye anaijua klabu vizuri sana.

Hamada Anwar (Timu Meneja, Zamalek)
Timu zote zilizofuzu ni mabingwa kutoka katika nchi zao. Natarajia tutakuwa na matokeo mazuri kutoka katika mchezo wa kwanza hivyo hatutakuwa katika presha katika mchezo wa marudiano.Tuna msimu mzuri na tunatarajia kushinda taji hilo.

Frederic Kitengie (Katibu Mkuu, TP Mazembe)
Ni ratiba nzuri kwetu. Katika kundi tuko na timu mbili zinashiriki kwa mara ya kwanza, ambazo ni Smouha na Moghreb Tetounae. Hizi zitatusumbua sana kwa sababu ni timu mpya hatuzijui vizuri.

Nimefurahi sana kuikwepa El Merreikh, ambayo inafundishwa na kocha wetu wazamani Diego Garzitto, ambaye anaijua vizuri timu yetu. Kundi jingine lina timu za Algeria dhidi ya Merreikh na ni vizuri tumeliepuka kundi kama hilo.

 Mohamed Ashraf (Rais, Moghreb Tetouane)
Ni vizuri tumezikwepa timu za Algeria. Ratiba inatupa nafasi angalau kucheza nusu fainali. Tunaangalia mbele kucheza na Smouha, kufuatia mapokezi mazuri tuliyoyapata wakati tumekwenda Misri kucheza dhidi ya Ahly.

Kwa sasa Sudan, nafikiri El Merreikh ni bora zaidi ya El Hilal, na hiyo itatuapa sisi nafasi. TP Mazembe ni timu imara sana katika kundi, lakini tuna nafasi.

No comments:

Post a Comment