Saturday 20 August 2016

Usain Bolt atwaa medali ya tisa ya dhahabu Jamaica ikishinda mbio za meta 4x100 kupokezana vijiti Michezo ya Olimpiki Rio 2016




Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt akivuka mstari na kushika nafasi ya kwanza.

RIO, Brazil
USAIN Bolt alimaliza kazi yake katika Olimpiki baada ya kutwaa tena medali tatu katika Olimpiki moja na kufikisha medali tisa za dhahabu wakati Mjamaica huyo aliposhinda fainali za mbio za kupokezana vijiti za meta 4x100 mjini hapa.

Bolt, 29, tayari alikuwa am,eshashinda mbio za meta 100 na 200 hapa na ndiye mtu pekee hadi sasa aliyewahi kushinda mbio zote fupi katika Olimpiki tatu.

Mwanariadha huyoa naungana na Asafa Powell, Yohan Blake na Nickel Ashmeade kumaliza kwa kutumia sekunde 37.27.

Japan ilipata medali ya kushangaza ya fedha huku Marekani ushindi wake watatu ukibatilishwa na kuifanya Canada kutwaa medali ya shaba na kuisogeza Uingereza hadi katika nafasi ya tano.

'Mwanariadha mkubwa'

"Kila uendapo. Mimi ni mkubwa," alisema Bolt, baada ya kumaliza kwa kushangaza historia yake ya Olimpiki katika kipindi chote.
 
Mwezi Februari, Bolt alithibitisha kuwa atastaafu baada ya mashindano ya dunia ya riadha yatakayofanyika jijini London mwakani na hatashiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020, ambapo atakuwa akikaribia umri wa miaka 34.

Umwamba wake wa kutwaa medali tisa za dhahabu anaungana kuwa miongoni mwa wanariadha wakubwa waliowahi kufanya hivyo wakati wengine ni mkimbiaji wa mbio fupi wa Marekani na mruka chini Carl Lewis na Mfiland anayekimbia mbio ndefu Paavo Nurmi.

Timu ya Marekani iliyoundwa na Mike Rodgers, Justin Gatlin, Tyson Gay na Trayvon Bromell ilishangilia ushindi wa medali ya shaba kabla haijapokonywa.
 
Timu hiyo ilielezwa kuwa ilipokonywa ushindi huo watatu kwa sababu Gatlin alipokea kijiti mapema kutoka kwa Rodgers wakati akipokea kwa mara ya kwanza, lakini wamekata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

No comments:

Post a Comment