Tuesday 30 August 2016

TTCL ndio wadhamini wakuu Miss High Learning 2016 watoa shilingi milioni 20 kwa shindano hilo




Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Mawasiliano Tanzania (TTCL) imetoa sh. Milioni 20 ili kudhamini shindano la kumsaka Miss Elimu ya Juu litakalofanyika Oktoba 17 katika ukumbi wa Sigara, Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Warembo wa shindano hilo leo Jumanne wametembelea Makao Makuu ya TTCL na kushuhudia shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo inayomilikiwa na Serikali, ambayo imepania kufanya mambo makubwa katika sekta ya mawasiliano hapa nchini.

Akizungumza katika ukumbi wa mikutano wa kampuni hiyo ya mawasiliano muandaa wa shindano hilo, Maya Nkini alisema kuwa jumla ya warembo 25 kutoka vyuo mbalimbali nchini wako kambini kujiandaa na shindano hilo, ambalo linatarajia kuwa na ushindani wa hali ya juu sana.

Nkini aliushukuru uongozi wa kampuni hiyo kwa kudhamini shindano hilo, ambalo sasa litajulikana kama “TTCL Miss Elimu ya Juu 2016”.

Muandaaji wa shindano la Miss Elimu ya Juu nchini,Maya Nkini akizungumza na waandishi wa habari leo.
Aliwataja wadhamini wengi kuwa ni pamoja na Time, Darling, AJ Events, ambao pia ndio waandaaji wa shindano hilo wakati wengine ni Radio E FM, Hussein Pamba Kali na  wengine.

Alisema kuwa washindi watatu wa kwanza watakata tiketi ya kushiriki katika shindano la Miss Tanzania 2016 litakalofanyika baadae mwaka huu.

Manager Customer Care wa TTCL, Aron Msonga.
Naye Maneger, Customer Care wa TTCL Aron Msonga aliwaelezea warembo hao kuhusu shughuli na mikakati ya mizima ya kampuni hiyo kuhakikisha inarejea kwa kishindo katika sekta ya mawasiliano nchini na tayarri imefanya mambo kibao.

Mmoja wa waratibu wa Miss Tanzania, Mr. Makoye akizunumza leo wakati warembo wa Miss Vyuo vya Elimu ya Juu walipotembelea TTCL. Wengine pichani ni muandaaji wa shindano hilo, Maya Nkini na Junior Makoye.
Mmoja wa waratibu wa Miss Tanzania Makoye alisema kuwa wamepokea kwa mikono miwili udhamini huo wa TTCL kwa Miss Elimu ya Juu na kuwaambia kuwa milango iko wazi kwa kampuni hiyo kuingia katika Miss Tanzania.
Warembo wakigawiwa kadi za Simu za TTCL na Manager Cutomer Care, Aron Msonga.
 Alisema kuwa TTCL imeonesha mfano kwa makampuni mengine kwa kudhamini shindano hilo na wao (Miss Tanzania) hawatawaangusha.

Warembo wote pamoja na viongozi wao waligawiwa line za simu za 4G zenye muda wa maongezi.








Meneja msaidizi wa TTCL mkoa  Kituo cha Dar es Salaam, Augustino Mwakyembe akiwapa maelezo warembo wa Miss Vyuo vya Elimu ya Juu nchini walipotembelea ofisi za kampuni hiyo ya mawasiliano mapema leo Jumanne.
 
Makoye akiteta na muandaaji wa Miss Vyuo vya Elimu ya Juu, Maya Nkini.

No comments:

Post a Comment