Tuesday 16 August 2016

Joao Havelange, Rais wazamani wa Fifa afariki dunia akiwa na umri wa umri wa miaka 100





ZURICH, Uswisi
RAIS wazamani wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa), Joao Havelange (pichani), amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100.

Mbrazil huyo nafasi yake ilichukuliwa na Sepp Blatter katika chombo hicho cha soka, ambapo alikitumikia kuanzia mwaka 1974 hadi 1998.

Pia alijiuzulu kama rais wa heshima wa Fifa Aprili mwaka 2013 kufuatia uchunguzi kuhusu madai ya rushwa dhidi yake, ambapo mwaka uliofuata alilazwa hospitalini kutokana na maambikizo katika mapafu.

Wakati wa uhai wake alikuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kuanzia mwaka 1963 hadi 2011, alijiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya.

"Alikuwa na wazo moja kichwani mwake ni kuufanya mchezi wa soka kuwa mchezo wa ulimwengu mzima huku kauli mbiu yake ikiwa ‘soka ni mchezo wa wote’ ,alisma mbadala wake Sepp Blatter.

Havelange aliiwakilisha Brazil katika mchezo wa kuogelea katika Michezo ya Olimpiki ya 1936, mwaka ambao alifuzu kuwa mwanasherria, kabla hajachaguliwa IOC.

Akiwa rais wa fifa aliongeza timu zinazoshiriki fainali za Kombe la Dunia kutoka 16 hadi 32, ambapo fainali sita zolifanyika chini yake.

Hatahivyo, historia yake ya soka ilichafuliwa na madai ya rushwa.

Kujitoa kwake katika IOC miaka mitano iliyopita akiogopa uchunguzi wa madai ya ISL, ambayo Havelange alikanusha tuhuma hizo.

No comments:

Post a Comment