Tuesday 9 August 2016

Bondia wa Namibia ashikiliwa kwa madai ya kutaka kubaka katika kijiji cha Olimpiki Rio de Janeiro, Brazil




Bondia Jonas Junius akiongoza timu ya Namibia katika ufunguzi wa Michezo ya 31 ya Olimpiki jijini hapa Ijumaa iliyopita.
RIO, Brazil
BONDIA wa Namibia Jonas Junius amekamatwa kuhusiana na vitendo vya ubakaji katika Kijiji cha Olimpiki, Polisi wa hapa wamethibitisha hilo.

Junius, ambaye ni bondia wa uzito wa light-welter, ambaye alikuwa apigane na Hassan Amzile katika raundi ya kwanza kesho Alhamisi, alishikiliwa baada ya kudaiwa kujaribu kumkumbatia na kumbusu mwanamke mmoja.

Ilidaiwa kuwa tukio hilo lilitokea Jumatatu usiku na Junius, ambaye ndiye aliyebeba bendera ya taifa ya Namibia wakati wa ufuguzi wa michezo hiyo Ijumaa usiku, alichukuliwa na kupelekwea katika kituo cha karibu cha polisi huko Recreio kwa mahojiano zaidi.

Taarifa ya polisi iliyotolewa katika mtandao ilisema: "Recreio ilisema jana, Agosti 7, kuwa Jonas Junius alikamatwa.

"Jonas alijaribu kunyakulia na kumpiga busu mwanamkeTukio hilo lilitokea katika gholofa ya 11 katika jengo la pili la Kijiji cha Olimpiki.

Chama cha Kimataifa cha Ngumi (AIBA), chombo cha ngumi za ridhaa, kina taarifa ya suala hilo.

Msemaji wa AIBA alisema: "AIBA inalichukulia suala hilo kwa umakini mkubwa kuhusu bondia huyo wa Namibia ambaye alitakiwa kushindana katika Olimpiki ya Rio 2016.

Endapo atashtakiwa, mthumiwa huyo atashikiliwa katika gereza la Bangu, ambako Mmorocco Hassan Saada amekuwa akishikiliwa tangu Ijumaa.

Saada anashtakiwa kwa tuhuma za kujaribu kubaka wafanya usafi wawili katika Kijiji cha Olimpiki, baada ya kumngangania mmoja, Jumatano.

No comments:

Post a Comment