Tuesday, 16 August 2016

Mbio za kilometa 21 za Kili FM International Marathon zaanza kwa kishindo mjini Moshi

 
Wanariadha wakianza mchuano katika mbio za nusu Marathon za Kimataifa za Kili FM zilizofanyika Moshi mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi Wetu, Moshi
HATIMAYE lile tukio lililokuwa likisubiriwa na wakazi wengi wa mji wa Moshi na maeneo ya jirani, Kili FM International Marathon limefanyika jana, huku Watanzania na Wakenya wakiwania ufalme wa mbio hizo za kwanza kufanyika na kuvutia mamia ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi.

Tofauti na miaka ya hivi karibuni ambako Watanzania wamekuwa wanyonge nyumbani mbele ya Wakenya, jana  walikataa kuendeleza uteja na kupambana vilivyo, hasa katika mbio za kilometa  21, ambapo Gabriel Gerald alitwaa ubingwa kwa upande wa wanaume.

Baadhi ya washiriki wa mbio za kilometa 21 kwa upande wa wanawake wakichuana jirani na mashamba ya miwa ya kiwanda cha Sukari cha TPC Moshi.
Gabriel Gerald, kijana anayekuja juu hivi sasa hapa nchini, alipeperusha vema bendera ya Tanzania baada ya kuwapiku Wakenya na washiriki wengine na kukamata nafasi ya kwa wanaume akitumia saa 1:05.05. Kwa ushindi huo, alijinyakulia kitita cha sh 700,000 na medali ya dhahabu.
Mkenya Kennedy Kimathi, alimaliza wa pili kwa akitumia saa 1:05.29 wakati nafasi ya tatu ilikwenda kwa mkonwe Dickson Marwa wa Tanzania aliyetumia saa 1:05.34.
Washindi wa pili na watatu kila mmoja aliondoka na zawadi ya sh 500,000 wakati nafasi ya nne ilikwenda kwa mwanariadha wa Kenya, David Kilimo aliyetumia saa 1:06.02 wakati watano ni Mtanzania, Agustino Sule aliyetumia saa 1:06.17.
Kwa upande wa wanawake Wakenya walijitutumua na Nancy Kiprop aliyetumia saa  1:15.00, nafasi ya pili ikitwaliwa na Mtanzania Magdalena Crispin kutoka Ausha aliyetumia saa 1:15.03 akifuatiwa na mwenzake Failuna Abdi pia Arrusha saa 1:16.0 huku nafasi ya nne ikichukuliwa na Angelina Tsere 1:16.36 wakati nafasi ya tano ikaenda kwa ladis Chepoi kutoka Kenya saa 1:17.0.
Wakichuana katika mbio za kilometa tano za kujifurahisha.
Katika mbio hizo zilizodhaminiwa na Radio Kili FM chini ya Mkurugenzi wake, Deo Lekule, washindi wa kwanza hadi 20 wote walipata zawadi na kuwa mbio ya kwanza kulipa washindi wengi.
Kwenye mbio za Km 5 zilitawaliwa na Watanzania ambako nafasi ya kwanza kwa wasichana ilikwenda kwa Cecilia Ginoka wa Arusha aliyetumia dakika 19:38.29 akifuatiwa na Amina Mohamed 20:31.94 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Angel John 20:58.2 wote kutoka Arusha.
Nafasi ya nne ilienda kwa mwanariadha wa siku nyingi Banuelia Brighton wa Kilimanjaro aliyetumia dakika 21:0582 huku mshindi wa tano akiwa ni Asma Rajab wa Arusha akitumia dakia 21:05.82.
Mshindi wa kwanza wa mbio za kilometa 21 kwa wanawake, Nancy Kiprop akizungumza na waandishi wa habari
Kwa upande wa wanaume mshindi aliibuka Faraja Thomas aliyetumia dakika 15:445.15 akifuatiwa na Josephat Joshua 1:47.70 wa tatu Sylivester Simon 15:49.43 wa nne mkongwe Msenduki Mohamed 15:49.86 hukju nfasi ya tano ikienda kwa Lukinga James 16:27.70.
Kwa upande wa mbio za watoto Km 2.5 wavulana, mshindi aliibuka Rashid Naasi wa Police Line Moshi aliyetumia dakika 9:35, wa pili Japhari Abdul wa Pasua 9:43 wa tatu Loloo Yusuph 10:10:35 kutoka Amani huku wa nne akiwa ni Nickson Patrick 10:45 wakati wa tano akiibuka ni Mathayo Jiange dakika 10:54 wote kutoka Amani.
Km 2.5 wasichana mshindi aliibuka Raphia Twalib kutoka Kikavu dakika 12:03, wa pili Getruda Talalai 12:12 wa Amani, wa tatu Hadija Alpha wa Majengo 12:17 huku wan ne akiibuka Lulu Shaba wa Mbuyuni 12:22 wakati nafasi tano ilienda kwa Grace Gastone kutoka Mwereni dakika 12:30.
Akizungumza katika mbio hizo, Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavala, mbali na kuipongeza Kili FM radia kwa kuamua kuwekeza katika mchezo wa riadha, aliwataka wakazi wa Moshi kuzidi kushirikiana na waandaaji hao kuendeleza tukio hilo linalochangia kukua kwa vipaji vya riadha hapa nchini.
Mkurugenzi wa Radio ya Kili FM, Deo Lekule, ambaye pia ndiye muandaa na mdhamini mkuu wa mbio hizo akifuatilia kwa makini wakati wa utoaji wa zawadi baada ya mbio hizo.
Aidha, Zavala, aliwaonya wakimbiaji kutoka nje ya nchi kuzingatia kuwa na mialiko maalumu kutoka kwenye mashirikisho yao wanapokuja hapa nchini, vinginevyo watazuiawa kushiriki.
Naye Mgeni rasmi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Wilbroad Mutafungwa, aliwapongeza waandaaji na kuahidi mbio zijazo jeshi la polisi litashiriki kikamilifu na ana uhakika watafanya vizuri.
Nani alisema Wachaga hawana ngoma? Ngoma ya Rosi, ambayo huchezwa wakati wa sherehe za Mangi nayo ilikuwepo kutumbuiza washiriki na watazamaji.
Alimtaka mwandaaji, kutokuona kama amepoteza kwa kile alichokifanya bali kina manufaa makubwa kwa jamii ya watu wa Kilimanjaro na maeneo mbalimbali.
Tukio hilo lilipambwa na burudani mbalimbali ikiwamo ngoma ya asili ya kichaga ya Rosi na muziki wa kizazi kipya kutoka kwa kundi la Mamong’oo kutoka Arusha, ambalo liliwakuna wengi.
 
Mbio hizo mbali na kuendeleza vipaji vya riadha ilikuwa na kauli mbiu ya mauaji ya walemavu wa ngozi, albino na ujangili, hususan mauaji ya tembo

 
Msanii Charles Frank au Nigger C wa Arusha akifanya vitu vyake wakati wa sherehe za kukabidhi zawadi  kwa washindi wa Kili FM International Marathon mjini Moshi.
 
Baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha Radio cha KIli FM wakiselebuka.

No comments:

Post a Comment