Tuesday, 9 August 2016

Mshahara wa Paul Pogba kufuru Manchester United kukomba mil 900 kwa wiki sawa na bil 3 kwa mwezi mmojaMANCHESTER, United
KLABU ya Manchester United imekamilisha rekodi ya dunia baada ya kumsajili Paul Pogba kwa pauni milioni 100.

Kiungo huyo anayehitajika zaidi duniani aliwasili hapa akitokea Juventus, na kujiunga tena na klabu hiyo ambayo aliondoka mwaka 2012.

Pogba, 23, anatarajia kuvalia jezi namba sita akiwa katika klabu hiyo, ambapo amesaini mkataba wa miaka mitano na atakuwa akilipwa kiasi cha pauni 290,000 (sawa na sh mil. 900) kwa wiki na atacheza chini ya kocha mpya wa timu hiyo Jose Mourinho.

Pia mkataba huo unaruhusu kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Akizungumza katika mtandao wa klabu hiyo, Pogba alisema: 'Nimefurahi kurejea Man United. Wakati wote ni klabu yenye nafasi maalum moyo mwangu na ninaangalia mbele kufanya kazi na Jose Mourinho.

'Nilifurahia muda wangu nikiwa Juventus na nina kumbukumbu za ajabu katika klabu kubwa nikiwa na wachezaji marafiki zangu. Lakini nahisi huu ni muda muafaka wa kurejea Old Trafford.

'Wakati wote nimekuwa nikifurahia kucheza mbele ya mashabiki na siwezi kusubiri kutoa mchango wangu kwa klabu. Hii ni klabu muafaka kwangu kufanikiwa kila kitu…’

Paul Pogba akiwasili katika Uwanja wa Mazoezi wa Manchester United katika msafara wa magari  ya kifahari jana.
Kocha wa timu hiyo Jose Mourinho alimpongeza Pogba na kusema kuwa atafanya mambo makubwa katika kipindi chake hicho cha pili cha kuicheze klabu hiyo.

Aliongeza kusema: 'Paul ni mmoja wa wachezaji bora duniani na atakuwa sehemu muhimu ya timu ya Man United ninayotaka kuiunda kwa ajili ya baadae. Yuko vizuri na ni mwepesi, anafunga mabao.

'Akiwa na umri wa miaka 23, ana nafasi kubwa ya kufanya nafasi hiyo kuwa yake katika kipindi cha miaka mingi. Bado ni kijana mdogo na bila shaka ataendelea kuimarika, na ana nafasi ya kuwa katika moyo wa klabu kwa muongo ujao na hata zaidi.

Pogba alitupia katika akaunti yake ya Instagram: ‘Niliondoka Manchester wakati nikiwa na umri wa miaka 18 ulikuwa uamuzi hiari kati ya klabu na mimi na sasa ni muda wa kurejea tena klabuni Old Trafford!

‘Ninaheshima kubwa kwa klabu ambazo zinajali kuwa na mimi.
Juventus wakati wote itakuwa sehemu yangu na siku zote nitaimisi, nitaipoenda na naifurahia klabu hiyo na hasa mashabiki wake. Nategemea wataheshimu uamuzi wangu.

‘Ni vigumu kuelezea sana katika mistari mifupi lakini nilifanya uamuzi uliongozwa na moyo weangu na hakuna kingine zaidi ya hapo.

‘Uhamisho huu ulichukua muda mrefu kwa sababu ni mkubwa na wenye mambo mengi.

Kwa ada hiyo, Pogba sasa ndiye mchezaji soka ghali zaidi, ambapo uhamisho wake wa kwenda United unauzidi ule wa pauni milioni 86 ambao Real Madrid iliilips Tottenham ili kumnasa nyota wa Wales Gareth Bale mwaka 2013.
Paul Pogba akiwa ndani ya uzi wa Manchester United namba sita baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano wa kuichezea timu hiyo.
 

No comments:

Post a Comment