Tuesday, 16 August 2016

Askari tisa wa Uganda wafungwa kwa wizi wa mafuta nchini Somalia ambako wanalinda amaniMOGADISHU, Somali
ASKARI tisa wa Uganda ambao wanafanya kazi kama walinzi wa amani nchini hapa wamefungwa kwa kupatikana na hatia ya kushiriki katika mchongo wa kuiba mafuta, imeelezwa.

Taarifa ya Umoja wa Afrika (AU) imesema kuwa askati hao wamefungwa jela kati ya mwaka mmoja hadi mitatu na mahakama ya Uganda, iliyokaa nchini Somalia.

Maofisa hao ni pamoja na mameja wawili, walikamatwa katika zoezi maalum lililofanyika mwezi Juni.

Jeshi hilo la AU linapambana pamoja na Jeshi la Serikali ya Somalia dhidi ya Jeshi la Kiislamu la al-Shabab.

Hii ni mara ya kwanza kwa mahakama ya kijeshi inayohusiana na Kamati ta AU (Amisom) kukaa nchini Somalia tangu jeshi hilo liundwe miaka tisa iliyopita.

Askari hao tisa ni miongoni mwa wale 1 waliosimama mbele ya mahakama wakidaiwa kuuza mafuta ya Amisom kwa raia katika mji mkuu huo wa Somalia, Mogadisho, taarifa ya Amisom ilisema.

No comments:

Post a Comment