Friday 18 November 2016

TFF, TBF mbioni kukacha Mkutano Mkuu wa Uchaguzi TOC Dodoma 2016




 Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, TOC, Filbert Bayi (kulia).

Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) ni miongoni mwa vyama vichache vya michezo, ambavyo vimeshindwa kuthibitisha ushiriki wake katika Mkutano Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, imeelezwa.

Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa TOC, umepangwa kufanyika mjini Dodoma Desemba 10 na Novemba 4 ndio ilikuwa mwisho kwa vyama kuthibitisha kushiriki.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi alisema kuwa TFF na Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) vimeshindwa kuthibitisha kushiriki katika mkutano huo mkuu.

Alisema kuwa vyama au mashirikisho ya michezo inayoshindwa kufuata taratibu kama hizo za kuthibitisha kushiriki alafu baadae ndio wanavuruga utaratibu kwa kushiriki bila ya kuthibitisha.

Alisema endapo chama kinathibitisha kushiriki kuna wasaidia TOC kuwapangia majumbe malazi na taratibu zingine zikiwemo hata kuwaandaalia dokumenti mbalimbali za katika mkutano.

Aidha, Kamati ya Utendaji ya TOC inatarajia kufanya kikao cha mwisho kabisa cha Kamati ya Utendaji Desemba 25 Zanzibar kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu huo wa uchaguzi.

Wakati huohuo, Kamati ya Uchaguzi ya TOC imeanza kazi ya kupitia fomu za wale wote wanaotaka kugombea nafasi mbali mbali za uongozi.

No comments:

Post a Comment