Wednesday 9 November 2016

Mafunzo ya walimu wa mchezo wa kuogelea yaendelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya mkufunzi ya Kimataifa


Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Gulam Rashid akifungua mafunzo ya makocha wa mchezo wa kuogelea ngazi ya juu uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), Thauria Hassan Diria, Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhan Namkoveka na kushoto ni Noel kihunsi.

Na Mwandishi Wetu
MAKOCHA wa mchezo wa kuogelea wametakiwa kuzingatia mafunzo ili kwenda kuuendeleza mchezo huo katika maeneo wanakotoka.

Hayo yameelezwa na Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC,  Gulam Rashid wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku 10 ya maocha wa mchezo wa kuogelea hatua ya ju.
 
 Mratibu wa mafunzo ya kuogelea wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Muharami Mchume akizungumza wakati wa mafunzo hayo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kozi hiyo ilifunguliwa juzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo walimu 30 wanapata mafunzo hayo kutoka kwa mkufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la mchezo wa kuogelea (Fina), Joshua Neuloh wa Ujerumani.
Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi akizungumza wakati wa mafunzo hayo ya kuogelea.
 Rashid aliwataka makocha hao kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania kujifunza kwa makini na kupeleka ujuzi wao huko watokako ili kuuendeleza mchezo huo.

Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), Ramadhani Namkoveka alisema washiriki hao wanachukua mafunzo ya juu ya ufundishaji mchezo huo wa kuogelea.
 
Washiriki wa mafunzo hayo ni kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Zanzibar, Mwanza na Singida.

Neuloh akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo alisema kuwa yatawasaidia makocha hao kufundisha kitaalam kuogelea.
 
Naye makamu mwenyekiti wa TSA, Thauriya Diria alishukuru Olympic Solidarity kupitia Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kuwapatia mafunzo hayo ya ngazi ya juu ya kuogelea.

Alisema kuwa washiriki wengi ni walimu watasaidia kuueneza mchezo huo kuanzia chini kabisa na kusaidia kuenea kwa zaidi mchezo huo hapa nchini.
Mkufunzi wa mafunzo kwa makocha wa uogeleaji, Joshua Neuloh wakati wa mafunzo hayo.
Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi na Makamu mwenyekiti wa Chama cha Kuogelea (TSA), Thauria Hassan Diria.




 

No comments:

Post a Comment