Saturday, 26 November 2016

Mwanamapinduzi FIDEL Castro wa Cuba afariki dunia akiwa na umri wa miaka 90HAVANA, Cuba
FIDEL Castro, rais wazamani wa Cuba na kiongozi wa mapinduzi ya kikomusti, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90.

Akitangaza kifo hicho mdogo wake, ambaye ndiye rais wa sasa wa Cuba, Raul Castro alisema mauti yalimkuta usiku.
"Kiongozi wa mapinduzi ya Cuba alimafikiri dunia usiku huu, alisema Rais huyo wa sasa wa cuba.

Fidel Castro aliiongoza Cuba nchi ya chama kimoja kwa zaidi ya miaka 50 kabla Raul hajaichukua mwaka 2008.

Mashabiki wake walisema aliirejesha nchi kwa wananchi. Lakini pia alitumuhumiwa kuukandamiza upinzani.

Kuanzia sasa kutakuwa na siku kadhaa za maombolezo ya kitaifa kutoka na msiba huo.

No comments:

Post a Comment