Saturday, 24 September 2016

Manchester United yaifunga Leicester City 4-1 wakati Paul Pogba akifungua akaunti yake ya mabao
Kiungo Mfaransa wa Manchester United, Paul Pogba (kulia) akikimbizwa na kiungo Muingereza wa Leicester City, Danny Drinkwater wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya England uliofanyika leo mchana kwenye Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester, kaskazini magharibi ya London. Man United ilishinda mabao 4-1.

LONDON, England
TIMU ya Manchester United leo mchana imeutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford baada ya kuwafunga mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England Leicester City kwa mabao 4-1.

Wakati timu hiyo ikiibuka na ushindi mnono, kocha Jose Mourinho amuacha kando ya kikosi cha kwanza nahodha wake Wayne Rooney.

Chris Smalling ndiye alikuwa wa kwanza kuipatia bao Man United kabla Juan Mata hajafunga la pili na kuifanya timu hiy kuongoza kwa mabao 2-0.

Marcus Rashford na Paul Pogba jana walifunga mabao yao ya kwanza katika timu hiyo, ambapo yote yalifungwa kwa njia ya kona.

Mabingwa watetezi Leicester City wenyewe walipata bao lao la kufutia machozi lililofungwa na Demarai Gray kwa shuti la mbali.

Rooney aliingia uwanjani katika dakika ya 83, ambapo hii ni mara ya kwanza nahodha huyo akiingia akitokea benchi tangu Desemba 26, 2016.

No comments:

Post a Comment