Saturday 10 September 2016

Bonanza la uzinduzi wa Mashindano ya Shimiwi 2016 lafana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Jumamosi



Washiriki wa Bonanza la uzinduzi wa mashindano ya Shimiwi wakipita katika barabara ya Mandera leo kuelekea Uwanja wa Uhuru.

Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu Kiongozi,  Balozi John Kijazi leo alikuwa mgeni rasmi katika Bonanza la uzinduzi wa mashindano ya 34 ya Shirikisho na Taasisi za Umma (Shimiwi), lililofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Utumishi, Lauriane Ndombaro akimkabidhi Kombe la ushindi wa kwanza Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva.
Kijazi ambaye hotuba yake ilisomwa na Katibu Mkuu wa Utumishi, Dkt Laurean Ndumbaro, ambayo iliwataka waajiri kuwatimizia mahitaji wafanyakazi wao ili waweze kujiandaa na kushiriki vizuri katika mashindano ya Shimiwi, ambayo mwaka huu yatafanyika Dodoma baadae mwezi ujao.

Alisema  kuwa waajiri wanatakiwa kuwa patia mahitaji muhimu kama vifaa vya michezo na mahitaji mengine ili wafanyakazi wao waweze kushiriki vizuri katika mashindano hayo, ambayo mwaka jana hayakufanyika ili kupisha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabune na Madiwani hapa nchini.
Dokta Mtaka akimchua mmoja wa washiriki katika bonanza hilo la ufunuzi wa Shimiwi leo Jumamosi.
 Kijazi pia alimpongeza Rais wa awamu ya tano wa Tanzania Dkt Pombe Maufuli kwa jitihada zake za kuliletea maendeleo ya haraka taifa la Tanzania, ambapo hadi sasa amefanya mambo mengi.
Pia aliwataka wafanyakazi hao wa umma kuwa na nidhamu wakati wote wa mashindano hayo ili kuonesha taswira nzuri kwa jamii.

Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakifanya mazoezi katika bonanza hilo leo.
Pia aliwataka wafanyakazi hao wa umma kufanaya mazoezi kila wakati sio kusubiri tu wakati wa bonanza hilo au mashindano ya Shimiwi kwani mazoezi uwajena kimiili na kiakili na kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
 
Aliwaambia kuwa michezo inawaepusha wafanyakazi hao wa Serikali na maonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu, kisukari, kupooza na mengine mengi.

Katika bonanza hilo viongozi mbalimbali wa wizara na taasisi mbalimbali za Serikali walishirriki katika bonanza hilo ambalo lilianza kwa washiriki zaidi ya 2,000 kukimbia katika mitaa mbalimbali ya jirani na Uwanja wa Uhuru na kurudi katika uwanja huo ambako walifanya mazoezi ya viungo kabla ya mgeni rasimu kuzungumza.
Mbali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Elisante Ole Gabriel, viongozi wengine waliokuwemo uwanjani hapo leo ni pamoja na katibu mkuu wa uchukuzi Dkt. Leornard Chamuriho (kulia) na katibu mkuu wa Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora.
 

Aidha, Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam (RAS) ndio ilitwaa ushindi wa kwanza katika shindano la taasisi iliyoshirikisha wafanyakazi wake wengi katika bonanza hilo la uzinduzi wa mashindano ya 34 ya Shimiwi baada ya kuwa na wafanyakazi 180 huku Kilimo walimaliza wa pili kwa kuwa na wafanyakazi 82.

Mwakilishi wa Kilimo (kulia) akipokea Kombe la ushindi wa pili kutoka kwa Katibu Mkuu Utumishi.
Washindi hao wa kwanza na pili walipewa zawadi ya makombe, ambayo yatakuwa yao kabisa.
Naye mwenyekiti wa Shimiwi Daniel Mwalusambi aliwashukuru viongozi wote waliowaruhusu wafanyakzi wao kushiriki bonanza hilo la uzinduzi wa mashindano ya Shimiwi.
 
Pia aliwataka kuwawezesha na kuwaruhusu kushiriki mashindano ya Shimiwi mkoani Dodoma mwaka huu.
Mwenyekiti wa Shimiwi, Daniel Mwalusambi akizungumza leo kwenye Uwanja wa Uhuru
MC wa Bonanza hilo la uzinduzi, ambalo lilifana, Joyce  Benjamin.

No comments:

Post a Comment