NOUAKCHOTT, Mauritania
KOCHA wa Mauritania Corentin Martins (pichani) hana uhakika wa kuendelea
kuwepo katika timu hiyo licha ya kuiongoza kumaliza vizuri hatua ya kufuzu ya
Mataifa ya Afrika (Afcon 2017).
Sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Afrika Kusini huko Nelspruit kuliihakikishia
Mauritania kumaliza katika nafasi ya pili katika kundi lake.
Wamekosa nafasi ya kufuzu kwenda Gabon mwakani lakini Martins alisema
kuwa kundi lao, ambapo pia likuwa na timu za Afrika Kusini na Gambia, lilikuwa
moja ya makudni ya kifo.
Mchezaji huyo wazamani wa Ufaransa, ambaye timu yake ilikuwa na
nafasi finyu kimahesabu ya kufuzu kwa fainali hizo kama ingeshinda mchezo huo,
alisema alikuwa akitarajia kumaliza wa pili katika msimamo wa kundi lao.
"Kwan chi ambayo haija wachezaji wengi wenye uzoefu katika
soka la kimataifa, tumepiga hatua kubwa, “alisema
kiungo huyo wazamani wa Auxerre.
"Zaidi ya miaka miwili, tulikuwa na nafasi kucheza na timu
kutoka mataifa makubwa kisoka Afrika na kujifunza mengi kutoka kwa wazoefu.
Ilikuwa nafasi finyu kwa Mauritania kupata nafasi kama ile ya kucheza na timu
kubwa.
"Kufanya vizuri dhidi yao tulitupatia kujiamini sana. Mara
mbili tumeshindwa kwa bao moja na Cameroon, na tulifungwa kidogo na Tunisia katika
mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia na tulipata pointi nne kutoka kwa Afrika
kusini.
Nafikiri tunaweza kuendelea kupata matokeo mazuri.”
Mauritania kwa muda mrefu ilikuwa ikichukuliwa kuwa ni taifa dogo
katika soka lakini baada ya sare ya Ijumaa inatarajia kupanda viwango vya Fifa
na kwa mara ya kwanza kufikia katika 100 katika kipindi cha miaka 20.
"Kwa kweli tulikuwa tukifanya kazi kwa bidii kuongezea ubora
timu hii na ninafikiri tumesonga mbele kwa haraka sana, “alisema Martins.
Lakini kocha huyo mwenye umri wa miaka 47, ambaye alinza kazi yake
na Mauritania Oktoba miaka miwili iliyopita, alisema kuwa hajui kama atapewa
ofa nyingine ya kuendelea kuifundisha timu hiyo.
Mkataba wake wasasa unatarajia kumalizika Desemba mwaka huu.
"Nina furahia sana
kazi hii, watu wa hapa ni wazuri sana kwangu na nimekuwa na uhusiano mzuri na
uongozi. Bila shaka, sio kitu rahisi kuwa kocha wa timu ya taifa-unaathirika
sana unapokuwa katika benchi.”alitania
kocha huyo. “Lakini sijui kitu gani
kitatokea sasa.”
Mauritania ilipoteza mechi mbili tu kati ya sita za kundi lake la
M, ambapo ilimaliza ikiwa na point inane.
Katika mashindano ya kufuzu yaliyopita ilimaliza ya mwisho
kimsimamo, na haikuwahi kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika.
No comments:
Post a Comment