Tuesday 6 September 2016

Mbio za mbuzi kufanyika Jumamosi Septemba 10 na kutarajia kukusanya sh mil 120


Meneja wa Bia ya Kilimanjaro wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Pamela Kikuli akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo kwenye hoteli ya Southern Sun kuhuzu Mbio za Mbuzi zitakazofanyika Jumamosi. Kulia ni Meneja Maswaliano wa Tigo, Umi Mtiro. Kulia kwa Kikuli ni mratibu wa mbio, Karen Stanley, meneja masoko wa Coca Cola Nalaka Hettiarachchi na bosi kutoka Toyota-Tanzania, Eliavera Timoth.

Na Mwandishi Wetu
SHINDANO la Mbio za Mbuzi litakalofanyika Jumamosi jijini Dar es Salaam linatarajia kukusanya kiasi cha sh Milioni 120 kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali.
Fedha hizo zitatumika kusaidia watoto wenye saratani, kusaidia kliniki ya meno inayotembea na kuzisaidia jamii zenye shida mbalimbali nchini.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Pamela Kikuli akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu Mbio za Mbuzi. Kushoto ni mratibu wa mbio hizo, Karen Staley au Mama Mbuzi.
 Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana mmoja wa waratibu wa mbio hizo Karen Stanley alisema kuwa mwaka huu wanatarajia mbio hizo kuwa na msisimko wa aina yake katika viwanja vya The Green Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Alisema mbio za mwaka huu zimedhaminiwa na Swiss Air, hoteli ya Southern Sun, Coca Cola, Toyota-Tanzania na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Umi Mtiro akizungumza katika hafla hiyo leo katika hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam. Kushoto ni meneja wa Bia ya Kilimanjaro Pamela Kikuli.
Swiss Air imesema itanunua tiketi 1,000 na kuziuza, ambapo katika tiekti hizo watacheza bahati nasibu na mshindi wawili, mmoja atapata tiketi ya daraja la pili kwenda Ulaya na nyingine kwenda mahali kokote duniani.

 Tangu kuanza kwa mbio hizo miaka 16 iliyopita tayari zimeshakusanywa zaidi ya sh Bilioni 1, ambazo zimesaidia miradi mbalimbali nchini kote ikiwemo ujenzi wa madarasa.

Mwalimu wa shule ya Muhogolo wa shule ya St. Paul English Medium ya Kibaigwa alisema mbio za Mbuzi zimesaidia shule pesa za kujenga madarasa.

Mwakilishi wa Toyota-Tanzania katika mbio za Mbuzi, Eliavera Timoth akizungumza leo katika hafla hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Umi Mtiro alisema kuwa wamekuwa wakidhamini mbio hizo kwa miaka miwili sasa, ambapo pamoja na mambo mengine wamekuwa wakitoa huduma ya mawasiliano uwanjani hapo.
Meneja Masoko na Mauzo wa Coca Cola nchini, Nalaka Hettiarachich akizungumza leo.
Mwaka jana mbio hizo ziliusanya kiasi cha sh Milioni 150, ambapo mwaka huu watakusanya pungufu ya mil 30 kutokana na ukata kwa baadhi ya makampuni.

No comments:

Post a Comment