Sunday 11 September 2016

Bingwa wa Olimpiki Mo Farah abaguliwa na mfanyakazi wa Shirika la Ndege la Delta wakati akitoka Rio



LONDON, England
BINGWA wa Olimpiki wa mbio za meta 5,000 na 10,000 Mo Farah alijikuta katika wakati mgumu baada ya kubaguliwa na mfanyakazi wa ndege na kurudisha nyuma katika mstari kabla ya kupanda ndege kwenda Marekani, alisema mke wake.

Tania Farah alisema mfanyakazi wa Shirika la Ndege la Delta alimtilia ngumu bingwa huyo mara nne wa medali za dhahabu za Olimpiki na kugoma kabisa kuamini kama mwanariadha huyo ana tiketi ya daraja la pili (business class).

Hatahivyo, taarifa zingine zilisema kuwa Farah na familia yake hiyo walichelewa kupanda ndege wakati abiria wa daraja la kwanza walipokuwa wakiingia katika ndege.

Msemaji wa Delta Airlines alisema baadae kuwa wanachunguza madai hayo na "watalifanyia kazi moja kwa moja kwa kushirikiana na familia hiyo ya Farah".

Tukio hilo inadaiwa lilitokea Agosti 22 wakati wawili hao pamoja na watoto wao wanne wakirejea kutoka katika Olimpiki ya Rio 2016, ambako Farah alitetea mataji yake yam bio za meta 5,000 na 10,000.

Farah na familia yake walikuwa katika hatua za mwisho za safari yao kutoka Atlanta kurudi kwao Portland, Oregon.

"Najua alikuwa na tatizo na yeye, alisema.Tania Farah katika gazeti la Jumapili la Telegraph, akimnukuu mfnayakazi huyo wa Delta Airlines.

"Huyu manamke alimdharirisha hadi watu walipokuja na kusema: 'Huyi ni Mo Farah, ni bingwa wa Olimpiki,alisema mke wake.

Farah, 33, alitarajia kuwa mtu wa kwanza kushinda mara tatu mfululizo mbio za Great North Run wakati wa mbio hizo Newcastle leo Jumapili.

No comments:

Post a Comment