Monday, 21 March 2016

Obama atua Havana,Cuba kwa ziara ya kistoriaRais wa Marekani, Barack Obama akisalimia na baadhi ya wafanyakazi na familia zao nchini Cuba.

HAVANA, Cuba
RAIS wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Cuba kwa ziara ya kihistoria katika kisiwa hicho na kuzungumza na kiongozi wa Kikoministi.

Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa rais wa Marekani kutembelea Cuba tangu yalipofanyika Mapinduzi ya mwaka 1959.

Akizungumza wakati wa kufungua tena ofisi ya ubalosi wa Marekani jijini hapa, aliita ziara hiyo kuwa ni ya kihistoria. Pia alitumia muda fulani katika katika jiji hilo kongwe.

Obama alikutana na Rais wa Cuba Raul Castro, lakini hakukutana na mwanamapinduzi mstaafu Fidel Castro, na wawili hao watazungumzia pia masuala ya biashara na mabadiliko ya siasa.

Rais huyo wa Marekani alitoka katika ndehe yake ya Air Force One akiwa na mkewe Michelle na watoto wake wawili wakike Sasha na Malia.

Akiwa ameshikilia mwamvuli, wawili hao walitembea wakielekea katika zuria jekundu akisalimiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Bruno Rodriguez.
  
"Tukirejea nyuma mwaka 1928, Rais [Calvin] Coolidge alikuja hapa kwa meli ya kivita. Ilimchukua siku tatu kufika hapa, lakini mimi imenichukua saa tatu tu, Air Force One kutua Cuba na hii ni kituo chetui cha kwanza tangu tulipopaa.

Baadae Obama alianza kutembelea jiji la zamani la Havana.

No comments:

Post a Comment