Wednesday 2 March 2016

Mrisho Mpoto kuzindua video ya Sizonje Jumamosi Machi 05,2016



Muimbaji Mrisho Mpoto (katikati), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa video ya Sizonje jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Masoko wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSPF, Magira Werema na meneja wa Mpoto Theatre,Maria Masome.
Muimbaji maarufu wa mashairi nchini, Mrisho Mpoto Jumamosi Machi 5, 2016 atazindua kibao chake kipya cha Sizonje katika ukumbi wa Golden Jubilee gholofa ya nne  jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mpoto, mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Mh. Waziri, wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye.

Alisema kuwa kabla ya uzinduzi huo kutakuwa na mjadala kuhusu Kufeli Elimu Sio Kufeli Maisha, ila kinachotakiwa ni kutokataa tamaa. Ikiwa na kauli mbiu ya INUKA ENDELEA

Alisema kuwa katika mjadala huo watu mbalimbali maarufu wakiwemo wasanii, wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Wahadhiri na wadau mbalimbali wa elimu watazungumza kuhusu suala la elimu,  hasa Kiswahili.

Mbali na watu hao pia wanatarajiwa kuwepo wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya Kiswahili katika kidato cha nne pamoja na baadhi ya wale, ambao hawakufanya vizuri ili kupata uzoefu wao na nini kifanyike ili kusonga mbele.

Aliwataja baadhi ya wasanii  na watu wengine maarufu watakaozungumza siku hiyo ni pamoja na Ruge Mutahaba, AY, Said Fella,  Niki wa Pili, Babu Tale, George Kavishe, Miss Tanzania Lilian Kamazima, Mbunge wa Mikumi Profesa Jay, Gardina, Shilole, Omyy Dimpoz na Mwana FA.

Alisema onesho hilo litafanyika katika ukumbi huo kuanzia saa 3:00 asubuhi.

Alisema kuwa kibao cha Sizonje ni elimu tosha ya Kiswahili, hivyo ni muhimu mjadala wa Kiswahili ukafanyika siku hiyo ya uzinduzi wake ili kuibua mjadala wa kitaifa.

Alisema kuwa wanafunzi waliofanya vibaya katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana ni wengi kuliko wale waliofaulu, hivyo ni muhimu kuwatia moyo ili kuhakikisha hawakati tamaa na badala yake wanasonga mbele na kuhakikisha wanafanya vizuri. Katika maisha.
 

Meneja Masoko wa Mfuko wa Jamii wa PSPF, Magira Werema akizungumza wakati wa kutangaza uzinduzi wa video ya Sizonje.
 
 

No comments:

Post a Comment