Saturday 5 March 2016

FA ENGLAND YAKATAA MPANGO WA KUANZISHWA KWA MASHINDANO YA SUPER CUP ULAYA



LONDON, England
MTENDAJI Mkuu wa Chama Soka England (FA), Martin Glenn amekanusha mpango wa kuanzisha mashindano ya Ulaya ya Super Cup, akisema kuwa yataua ushindani.

Klabu kubwa za Ligi Kuu wiki hii zilifanya kikao cha kujadili mpango wa kuwa na mashindano ambayo yatashirikisha timu kubwa za bara la Ulaya.

Lakini Glenn alisema kusimamisha ligi kwa ajili ya kuziwezesha baadhi ya timu kushiriki mashindano hayo kutawaweka kando mashabiki.

"Soka linatakiwa kuhusishwa (lakini) hatuwezi kupoteza misingi ya kupanda na kushusha timu, alisema Glenn.

Kocha wa Manchester United Louis van Gaal na yule wa Arsenal tayari wameweka wazi kupinga Super Leaguehiyo ya Ulaya.

Glenn, aliyechaguliwa mwaka mmoja uliopita, alitolea mfano vinara wa Ligi Kuu ya Leicester, ambao hawataweza kujiuna na timu hizo kubwa hata kama watashinda taji.

Aliongeza pia kusema jinsi mapato ya TV yanapogawanywa sawa kwa klabu kunaziwezesha timu kama Mbweha hao kuwa na kiwango walichonacho sasa.

Kikao hicho cha "siri" cha klabu kubwa tano za England kimezua madala. Martin Glenn ni `mzito wa hivi karibuni kukosoa mpango huo wa kuanzisha ligi hiyio ya Ulaya.

No comments:

Post a Comment