Sunday, 14 February 2016

Chelsea yaikung'uta Newcastle mabao 5-1
LONDON, England
KLABU ya Chelsea jana ilipata ushindi wa kwanza wa nyumbani wa  Ligi Kuu ya England chini ya kocha wa muda, Guus Hiddink kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya timu inayochechemea ya Newcastle.
Kikosi cha Hiddink kilichezea nyumbani mechi zake zote nne kwenye Uwanja wa Stamford Bridge tangu Mholanzi huyo achukue nafasi kutoka kwa mwenzake aliyetimuliwa Jose Mourinho kama kocha wa muda tangu Desemba.
Lakini Diego Costa ndiye aliyekuwa wa kwanza kuifungia Chelsea kwa bao la mapema kabla Pedro hajaongeza huku Willian na Bertrand Traore wakifunga na kuiwezesha timu hiyo kubuka na ushindi.
Mkosi katika mchezo huo uliibukia baada ya nahodha wa Blues John Terry kutoka nje ya uwanja baada ya dakika 37 kufuatia kuumia, kutokana na kugongana na Aleksandar Mitrovic.
Terry huenda asicheze mchezo wa Jumanne wa hatua ya 16 bora wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Paris Saint Germain (PSG).
Ushindi huo ni maandalizi mazuri ya Chelsea kwa mchezo huo muhimu dhidi ya PSG, ambapo Pedro alionesha mchezoi mzuri.
Kikosi cha kocha Steve McClaren kilionekana kuwa katika hatari ya kushuka daraja baada ya kuporomoka tena hadi katika nafasi ya tatu mkiani chini ya Norwich kwa tofauti ya mabao.

No comments:

Post a Comment