Sunday, 28 July 2019

Askari, Mbwa Kuongezwa Viwanja vya Ndege

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (kulia) akiongozana na maafisa wa ulinzi na usalama kukagua sehemu za kupitisha mizigo kwenye Jengo la tatu la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa la Julius Nyerere (JNIA TB3), alipofanya ziara hivi karibuni.

Na Mwandishi Wetu
Wizara ya Mambo ya Ndani nchini, itaongeza askari watu na mbwa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama kwenye viwanja vya Ndege nchini.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Hamad Masauni amesema hayo alipofanya ziara ya kikazi katika Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA TB3).

Masauni amesema serikali inatarajia kuongeza askari mbwa wengi wenye mafunzo na sifa, ili kuongeza ufanisi na ulinzi wa viwanja vyote vya ndege.

“Idadi ya mbwa inatakiwa iongezwe hasa inapokaribia kuhamia kwenye jengo jipya la tatu la abiria, ambalo litakuwa na idadi kubwa ya abiria na changamoto nyingi, pia kwa viwanja vingine navyo vitaangaliwa kwa suala la ulinzi,” alisema Masauni.

Hatahivyo, amesema hatasita kukifuta kitengo cha mbwa endapo hakutakuwa na mbwa wa kukidhi mahitaji na wenye sifa zote, kwani kwa sasa askari binadamu ni wengi zaidi.

Ametoa maelekezo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi  (IGP), Simon Sirro  kuhakikisha mfumo na ushiriki wa askari wake unaweza kuboreshwa na wale wanapelekwa viwanja vya ndege wawe na sifa na vigezo maalum vya kuweze kubaini vitu kama nyara za serikali, madini na  madawa ya kulevyia.

“Hii itasaidia kwa kuwa na mfumo wa pamoja wa ushirikiano katika udhibiti, jingine ni kuhakikisha IGP analisimamia na kulitekeleza kwa haraka sana, kwani tumekuwa na askari mbwa waliopata mafunzo maalum ya kubaini vitu mbalimbali vinavyopitishwa kwenye viwanja vya ndege, hivyo maelekezo yangu kwake tuongeze idadi ya mbwa wenye sifa hapa JNIA ili kufanya kazi kwa ufanisi zaidi,” alisema Masauni.

Masauni amefanya ziara hiyo siku moja baada ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kushughudia makabidhiano ya kilo 35.267 za dhahabu zilizokamatwa Februari 15, 2019 katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Jomo Kenyatta, Nairobi nchini Kenya.

Saturday, 27 July 2019

Real Yakiona cha Mtema Kuni, Yachapwa 7-3

Diego Costa, mfungaji wa bao nne pekee wakati Real Madrid ikifungwa 7-3 na Atletico Madrid.

NEW JERSEY, Marekani
DIEGO Costa alifunga mabao manne na alitolewa wakati Atletico Madrid ikiisambaratisha Real Madrid kwa mabao 7-3 jijini hapa.

Costa alifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya kwanza na kukamilisha hat-trick yake kwa bao la penalti alilofunga katika dakika ya 45.

Joao Felix, mchezaji aliyesajiliwa katika kipindi hiki cha majira ya joto kwa ada ya  pauni milioni 113, naye pia alifunga bao lake la kwanza katika klabu hiyo wakati Atletico ikiongoza kwa mabao 5-0 hadi mapumziko.

Costa alingeza la nne dakika sita baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, kabla ya yeye na mchezaji wa Real Dani Carvajal hawajatolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupigana katika dakika ya 61.

Angel Correa, aliyeingi aakichukua nafasi ya majeruhi Alvaro Morata, naye pia alizifumania nyavu katika kipindi cha kwanza, wakati Vitolo alifunga bao la saba kwa Atletico katika dakika ya 70.

Real waliendelea kuwa nyuma kwa mabao 6-0 kabla Real Madrid haijarekea katika ubao wa matangazo kwa mabao kupitia kwa Nacho, wakati Karim Benzema na Javier Hernandez wote wakifunga mabao katika dakika za majeruhi.

Gareth Bale, ambaye anajiandaa kuondoka Real Madrid na kujiunga klabu ya China ya Jiangsu Suning, alianzia katika benchi, lakini aliingia katika dakika 30 za mwisho.

Real, ambayo ilitumia kiasi cha pauni milioni 300 katika kipindi cha majira ya joto, ilianza kusajili kwa kumsajili Eden Hazard na Luka Jovic.

Lakini walipambana katika ziara yao ya Marekani kabla ya kuanza kwa ligi, ambapo walifungwa 3-1 na Bayern Munich na kuifunga Arsenal kwa penalti baada ya kutoka sare ya 2-2.

"Tulipoiangalia Madrid, tulikuwa tukiangalia wapi tutaimaliza, “alisema kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone. "Tulikuwa na muda mzuri hapa.”

Nahodha wa Real Sergio Ramos alisema: "Ni wazi hatuikuwa tukijisikia vizuri hapa. Na huu ndio mwanzo wa maandalizi yetu, Kuna njia nyingi zinazokufanya ushindwe, lakini hatuwezi kufanya kama tulivyofanya leo.

Kocha wa Real Zinedine Zidane aliongeza: "Hatuna haja ya kumtafuta mchawi katika hilo, hii ni mechi za maandalizi kabla ya kuanza kwa msimu mpya.


Bale Kulamba Bil 2.4 Kwa Wiki Akicheza China

MADRID, Hispania
GARETH Bale anakaribia kukamilisha uhamisho kutoka Real Madrid kwenda katika klabu ya China ya Jiangsu Suning kwa mkataba wa miaka mitatu utakaomuwezesha kuweka kibindoni mshahara wa pauni milioni 1 (sawa na sh bilioni 3) kwa wiki.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales, yuko katika hatua za mwisho za makubaliano na Jiangsu, ambao sasa wana uhakika wa kukamilisha usajili wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.

Endapo mpango huo utakwenda vizuri, basi Bale atakuwa amelamba dume kwa kupata karibu mara mbili ya mshahara wake wa pauni 600,000 kwa wiki ambao analipwa Real Madrid na atakuwa nyota mkubwa kujiunga na Ligi Kuu ya China.

Klabu ya Beijing Guoan nayo pia imeulizia kutaka kumsajili, lakini Jiangsu ndio inaonekana kushinda mbio hizo za kumpata mchezaji huyo.

Lionel Messi ndiye mchezaji soka anayelipwa zaidi duniani, ambapo kwa wiki anaondoka na karibu pauni milioni 1.7 katika Barcelona, na mkataba wa Bale pale  Jiangsu utamuwezesha kumkaribia mchezaji huyo wa Barca.

Chanzo cha karibu kabisa na mchezaji huyo wazamani wa Tottenham Hotspur kimeelezea ofa hiyo ya Jiangsu kama ni “isiyoelezeka”.

Bale alikuwa akijiandaa kung’ang’ania kubaki Real Madrid, licha ya kocha Zinedine Zidane kuweka wazi kuwa anamtaka mchezaji huyo kuondoka katika klabu hiyo, lakini taarifa zilizotolewa na Telegraph Sport, zinasema mchezaji huyo yuko tayari kwenda China.

Chanzo kutoka Hispania kinadai kuwa Bale atasaini mkataba wa miaka mitatu ndani ya saa kadhaa, ingawa marafiki wa mchezaji huyo Ijumaa walisema mpango huo bado haujakamilika vizuri.

Zidane alimaliza kipindi cha Bale Real Madrid baad aya mchezo wa kirafiki wa maandalizi uliofanyika Jumapili iliyopita dhidi ya Bayern Munich aliposema: 
“Hajamuhusisha mchezaji huyo katika kikosi chake wakati klabu hiyo ikifanyia kazi suala la kuondoka kwake, na ndio maana hakucheza.

“Tutaangalia nini kitatokea katika siku zijazo. Tunatakiwa kuangalia nini kitatokea kesho, endapo kitatokea, basi ni jambo zuri. Acha tuwe na matumaini kwa faida ya kila mmoja, na hilo litatokea haraka sana. Klabu inawasiliana na klabu nyingine…”

Wakala wa Bale, Jonathan Barnett aliendelea kusema kuwa Zidane “amekywqa amuheshimu” mteja wake, lakini kocha huyo ameendelea kusisitiza kuwa hali ya mshambuliaji hyo bado inabaki vile vile licha ya Marco Asensio kuendelea kuwa majeruhi kwa muda mrefu.

Zidane pia aliendelea kumbania Bale, huku akiendelea kuwa kimya bila kuelezea mcheaji huyo anataka nini.

Sasa inaonekana kipindi cha miaka sita cha Bale kukaa Real kimekaribia kumalizika na kuiacha klabu hiyo aliyotwaa nayo mataji manne ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na taji la La Liga.

Hiyo inamfanya Bale kuwa mwanasoka wa Uingereza mwenye mafanikio zaidi anayecheza soka nje hasa pale aliponunuliwa kwa rekodi ya ada ya pauni milioni 85 wakat akitua Real akitokea Tottenham mwaka 2013.

Dirisha la usajili China linatarajia kufungwa Jumatano ijayo, lakini Bale anatarajia kuwa mchezaji wa Jiangsu katika kipindi hicho na kuhamia kwake China kutamfanya kupata mapokezi ya kishujaa.

Kwa sasa Ezequiel Lavezzi ndiye mchezaji anayelipwa zaidi China kwa anapewa pauni 500,000 kajubu mkataba wa Bale utafunika huo wa Muargentina huyo.

Ni Kisasi Taifa Stars, Harambee Leo Uwanja wa Taifa

Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, wakijifua kwenye Uwanja wa Boko Veterani.

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inatarajiwa kucheza kesho dhidi ya timu ya taifa ya Kenya ‘Harembee Stars’ mchezo wa kwanza wa kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan 2020) utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo ni muhimu kwa Stars kuhakikisha inatumia vyema uwanja wa nyumbani kupata matokeo mazuri ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga raundi ya mwisho ya kufuzu. Timu hizo zitarudiana Agosti 4.

Stars inataka kulipiza kisasi hasa baada ya kufungwa katika mchezo wa makundi kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) Misri bada ya kuchapwa 3-2 licha ya kuongoza mara mbili.

Lakini mchezo wa leo utawahusisha wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani na Taifa Stars ndio inaonekana kuwa na faida zaidi baada ya kuwa na asilimia kubwa ya kikosi chake kilichoenda Misri kupata uzoefu mkubwa.

Iwapo watatumia vyema uwanja wa nyumbani watajitengenezea mazingira mazuri ya kufuzu.

Hatahivyo, Kenya sio timu ya kubeza kwani wako vizuri na wanataka kuutumia mchezo huo kupata matokeo ili kujiweka vizuri kwa ajili ya mchezo wa mwisho utakaofanyika Nairobi wiki ijayo.

Katika viwango vya ubora wa soka duniani bado Kenya wako vizuri ukilinganisha na Tanzania, wanashikilia nafasi ya 107, huku ndugu zao wakishika nafasi ya 137.
Kila mmoja ana nafasi ya kupata matokeo kulingana na alivyojiandaa dhidi ya mpinzani wake kimbinu.

Mchezo huo utakuwa ni mtihani wa kwanza kwa makocha Ettiene Ndayiragije na wenzake walioteuliwa kukaimu nafasi ya Emmanuel Amunike na Hemed Morocco.
Akizungumzia mchezo huo Kocha Ndayiragije alisema alisema jana kuwa maandalizi yote yako vizuri na kwamba kinachohitajika kwa wachezaji ni umakini kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

Nahodha John Bocco alisema mchezo huo utakuwa mgumu kwani kila mmoja atahitaji matokeo kujiweka katika nafasi nzuri, lakini anaamini kwa morali walionao watapambana kupata matokeo mazuri kwenye uwanja wa nyumbani.

Bocco aliwaomba Watanzania kutoenda uwanjani na matokeo yaliyopita bali sasa wako vizuri kulipiza kisasi kwa kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo.

Tanzania kwa mara ya mwisho ilishiriki fainali za Chan zilipofanyika Ivory Coast 2009 ikiwa ni miaka 10 sasa, hivyo itataka mwaka huu iweke rekosi tena kwa kufuzi fainali hizo.

Fainali za kwanza za Chan zilifanyika mwaka 2009 na lengo la Shirikisho la Afrika (Caf) ni kutoa nafasi kwa wachezaji ambao hawajasajiliwa nje ya nchi zao na kuwawezesha kujitangaza.

Ulinzi Kuimarishwa Viwanja vya Ndege Tanzania


 
 Mhandisi Burton Komba (wanne kulia) anayesimamia mradi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB3), akimweleza jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Hamad Masauni  (mwenye suti) alipotembelea jengo hilo hivi karibuni.


Na Mwandishi Wetu

Wizara ya Mambo ya Ndani nchini, itaongeza askari watu na mbwa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama kwenye viwanja vya Ndege nchini.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Hamad Masauni amesema hayo alipofanya ziara ya kikazi katika Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA TB3).

Masauni amesema serikali inatarajia kuongeza askari mbwa wengi wenye mafunzo na sifa, ili kuongeza ufanisi na ulinzi wa viwanja vyote vya ndege.

“Idadi ya mbwa inatakiwa iongezwe hasa inapokaribia kuhamia kwenye jengo jipya la tatu la abiria, ambalo litakuwa na idadi kubwa ya abiria na changamoto nyingi, pia kwa viwanja vingine navyo vitaangaliwa kwa suala la ulinzi,” alisema Masauni.

 Ofisa Usalama Mwandamizi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Ramadhani Mkumbukwa (aliyenyoosha mkono), akimweleza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (wapili kulia) namna ya ukaguzi wa abiria na mizigo unavyofanyika wakiwa kwenye jengo la tatu la abiria la JNIA hivi karibuni.

Hatahivyo, amesema hatasita kukifuta kitengo cha mbwa endapo hakutakuwa na mbwa wa kukidhi mahitaji na wenye sifa zote, kwani kwa sasa askari binadamu ni wengi zaidi.

Ametoa maelekezo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi  (IGP), Simon Sirro  kuhakikisha mfumo na ushiriki wa askari wake unaweza kuboreshwa na wale wanapelekwa viwanja vya ndege wawe na sifa na vigezo maalum vya kuweze kubaini vitu kama nyara za serikali, madini na  madawa ya kulevyia.

“Hii itasaidia kwa kuwa na mfumo wa pamoja wa ushirikiano katika udhibiti, jingine ni kuhakikisha IGP analisimamia na kulitekeleza kwa haraka sana, kwani tumekuwa na askari mbwa waliopata mafunzo maalum ya kubaini vitu mbalimbali vinavyopitishwa kwenye viwanja vya ndege, hivyo maelekezo yangu kwake tuongeze idadi ya mbwa wenye sifa hapa JNIA ili kufanya kazi kwa ufanisi zaidi,” alisema Masauni.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (mwenye suti), akionyesha jambo akiwa kwenye eneo la ukaguzi wa abiria na mizigo wakati alipotembelea jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa la Julius Nyerere (JNIA TB3) hivi karibuni.
Masauni amefanya ziara hiyo siku moja baada ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kushughudia makabidhiano ya kilo 35.267 za dhahabu zilizokamatwa Februari 15, 2019 katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Jomo Kenyatta, Nairobi nchini Kenya.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (kulia) akiongozana na maafisa wa ulinzi na usalama kukagua sehemu za kupitisha mizigo kwenye Jengo la tatu la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa la Julius Nyerere (JNIA TB3), alipofanya ziara hivi karibuni.


Thursday, 18 July 2019

STARS YAPANGWA NA TUNISIA, LIBYA NA GUINEA YA IKWETA MBIO ZA KUFUZU AFCON 2021 CAMEROON


CAIRO, Misri
TIMU ya taifa ya Tanzania imepangwa katika Kundi J pamoja na Tunisia, Libya na Guinea ya Ikweta, katika mbio za kuwania kufuzu kwa fainali zijazo za michuano ya Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Cameroon 2021.

Hilo limebainka baada ya Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) kupanga ratiba hiyo katika hafla iliyofanyika jijini hapa.

Katika kundi hilo la Tanzania na Tunisia ndizo pekee zilikuwepo katika fainali za mwaka huu ambazo zinamalizika kesho jijini hapa, kwa kuzikutanisha Algeria na Senegalm ambazo zote zimetoka katika Kundi C pamoja na Tanzania, huku Guinea ya Ikweta na Libya zilishindwa kufuzu.

Tunisia wenyewe ilifungwa na Nigeria 1-0 jana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Afcon 2019 Misri wakati Tanzania ilifungwa mechi zote tatu za Kundi C, ikiwa  2-0 na Senegal, 3-2 na Kenya huku Algeria ikiichapa Stars 3-0.
Kenya iliyokuwa kundi moja na Tanzania kwenye fainali za mwaka huu, yenyewe kwenye mbio za kusaka tiketi ya kwenda Cameroon 2021, imepangwa Kundi G pamoja na wenyeji wa mwaka huu Misri, Togo na Comoro.

Uganda wamepangwa Kundi B pamoja na Burkina Faso, Malawi na ama Sudan Kusini au Shelisheli, wakati Algeria imepangwa Kundi H pamoja na Zambia, Zimbabwe na Botswana na Senegal ipo Kundi I pamoja na Kongo, Guinea Bissau na Eswatini.

MAKUNDI YOTE KUFUZU AFCON 2021 CAMEROON

Kundi A: Mali, Guinea, Namibia, Liberia/Chad

Kundi B: Burkina Faso, Uganda, Malawi, Sudan Kusini/Shelisheli

Kundi C: Ghana, Afrika Kusini, Sudan, Mauritius/Sao Tome

Kundi D: DRC, Gabon, Angola, Djibouti au Gambia

Kundi E: Morocco, Mauritania, CAR, Burundi

Kundi F: Cameroon, Cape Verde, Msumbiji, Rwanda

Kundi G: Misri, Kenya, Togo, Comoro

Kundi H: Algeria, Zambia, Zimbabwe, Botswana

Kundi I: Senegal, Congo, Guinea Bissau, Eswatini

Kundi J: Tunisia, Libya, Tanzania, Equatorial Guinea

Kundi K: Ivory Coast, Niger, Madagascar, Ethiopia

Kundi L: Nigeria, Benin, Sierra Leone, Lesotho

Monday, 24 June 2019

Serikali Yaweka Mikakati Viwanja vya Ndege

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issac Kamwelwe leo akifungua Jukwaa la Pili la Kitaifa la Usafiri wa Anga linalofanyika kwa siku mbili kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema imeweka mipango kabambe ya kuboresha viwanja vidogo vya ndege (Airstrips), ili viweze kutumika kirahisi na ndege ndogo zinazosafirisha Watalii kutembelea mbuga mbalimbali za wanyama na vivutio vilivyopo nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issac Kamwelwe katika Jukwaa la Pili la Kitaifa la Usafiri wa Anga linaloendelea kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), ambapo tayari imeundwa kamati kutembelea viwanja hivyo, ambavyo amesema vipo zaidi ya 600 vikiwemo vya makampuni binafsi.

“Hivi viwanja ndivyo vinavyoingiza Watalii ndani ya mbuga na vivutio vingine baada ya kushuka pale KIA (Kilimanjaro International Airport) na hapa Dar es Salaam Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), sasa hivi vinatakiwa viwe katika ubora mzuri utakaofanya Watalii kujiona wapo sehemu nzuri na salama,” amesisitiza Mhandisi Kamwelwe.
Wadau mbalimbali wa masuala ya usafiri wa anga leo kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC),  wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi wa Jukwaa la Pili la Kitaifa la Usafiri wa Anga, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issac Kamwelwe.

Hata hivyo, Mhandisi Kamwelwe amesema Idara ya Uhandisi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), itaimarishwa zaidi ili iweze kufanya marekebisho kwenye viwanja hivi, ikiwezekana kununuliwa vifaa ili kufanya kazi kwa ufanisi.

Pia amesema tayari Serikali imeweza kusimamia vyema mradi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la abiria la JNIA, ambao umekamilika na limeongeza uwezo wa kuhudumia abiria, ambapo itahudumia abiria milioni sita kwa mwaka badala ya milioni 2 waliokuwa wakihudumia na Terminal 2.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Vedastus Fabian (kushoto) akiwasikiliza Maafisa Naomi Mbilinyi na Gladston Mlay (kulia), kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), katika maonesho yanayokwenda sambamba na Jukwaa la Pili la Kimataifa la Usafiri wa Anga linalofanyika kwa siku mbili mfululizo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC). 
“Ninawataka wafanyabiashara na wadau wengine wote kuchangamkia fursa za kibiashara zilizopo kwenye jengo letu hili la kisasa, ambapo sasa nimetaarifiwa wapo katika hatua za kuwapata watoa huduma ndio maana ninasema mjitokeze kwa wingi kuomba,” amesema Mhandisi Kamwelwe.
Dkt Bartholomew Rufunjo (kulia) leo akipata maelezo mbalimbali kuhusiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kutoka kwa Mhandisi Astelius John (kushoto), kwenye maonesho yanayokwenda sambamba na Jukwaa la Pili la Kitaifa la Usafiri wa Anga yanayofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC). Wengine pichani ni Afisa Masoko wa TAA, Pendo Mwakilasa akizungumza na Mtendaji Mkuu wa VIA Aviation Ltd, Suzan Mashibe.

Akizungumzia viwanja vingine amesema baada ya kukamilika kwa upanuzi na ukarabati wa viwanja vya ndege vya Songwe na Mwanza vitawekwa katika daraja la Kimataifa, kutokana na kuwa na miundombinu ya kisasa, ambapo kwa upande wa Mwanza ujenzi wa jengo la mizigo upo katika hatua ya mwisho kukamilika.

  1. Mhandisi Astelius John na Afisa Masoko, Pendo Mwakilasa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (kushoto), leo wakiwaeleza masuala mbalimbali ya viwanja vya ndege wadau waliotembelea meza ya maonesho yanayokwenda sambamba na Jukwaa la Pili la Kitaifa la Usafiri wa Anga yanayofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).
Kwa sasa kiwanja cha ndege cha Songwe kipo daraja 3C na yakikamilika maboresho ya miundombinu kitakuwa daraja la 4D na Mwanza ni daraja 4C.

Sunday, 16 June 2019

Mbwana Samatta Atakiwa Lazio Kwa Bilioni 41.2


ROME, Italia
NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, na mshambuliaji wa Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta ni mmoja mwa wachezaji waliotangazwa hivi karibuni kabisa kusakwa na Lazio kwa ajili ya usajili wa kipindi hiki cha majira ya joto.

Samatta alifunga mabao 20 katika mechi 28 alizocheza katika Ligi Kuu ya Ubegiji msimu uliopita, huku akisaidia mara tatu. Baada ya kusaini Genk akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ada ya uhamisho na kiasi cha sh bilioni 2, Samatta sasa ana thamani ya zaidi ya sh bilioni 30 na Lazio wako tayari kumchukua kwa sh bilioni 41.2.

Mkataba wa Samatta Genk unamalizika mwakani na itakuwa kazi kubwa kumchukua mchezaji huyo kumpeleka Rome katika kipindi hiki cha majira ya joto.

Lazio ni klabu ya Italia yenye maskani yake jijini Rome nchini humo, na inajulikana sana kwa shughuli zake za soka katika eneo hilo na inashiriki katika Ligi Kuu ya Italia ya Serie A.

Lazio imewahi kutwa taji la Ligi Kuu ya Italia mara mbili (mwaka 1974 na 2000), na wamewahi kushinda taji la Coppa Italia mara saba na mara nne lile la Supercoppa Italiana, na wamewahi kuwa mabingwa wa Kombe la Ligi ya Mabingwa pamoja na lile la Super Cup katika wakati mmoja.

Klabu kadhaa zinazoshiriki Ligi Kuu ya England, ikiwemo West Ham tayari zimeonesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wazamani wa Simba na TP Mazembe.


Saturday, 15 June 2019

Amunike Atamba Kutinga Raundi ya Pili Afcon 2019


CAIRO, Misri
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mnigeria Emmanuel Amunike (pichani) amesema kuwa kikosi chake kitafanya kila kitu kuhakikisha kinacheza raundi ya pili ya mashindano ya Mataifa ya Kombe la Afrika (Afcon 2019).

Licha ya kucheza vizuri katika safu ya ulinzi, timu hiyo ya Tanzania ilipoteza mchezo wake wa kimataifa wa kirafiki kwa kufungwa 1-0 dhidi ya Misri uliofanyika Alhamisi jijini Alexandria ukiwa ni mchezo wao wa kwanza wa kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa fainali hizo za Afcon 2019.

Fainali hizo za Mataifa ya Afrika zinafanyika nchini Misri kuanzia Juni 21 hadi Julai 19 na kwa mara ya kwanza zikishirikisha jumla ya timu 24 badala ya 16 za awali.

Tanzania inatarajia kucheza mchezo wake wa pili wa marudiano utakaofanyika leo Jumapili dhidi ya Zimbabwe, ikiwa ni wiki moja kabla ya kuanza kutimua vumbi kwa fainali hizo za Afcon 2019.

Taifa Stars imepangwa katika kundi gumu la C pamoja na vigogo wa Afrika, Senegal na Algeria pamoja na nchi jirani ya Kenya.

Amunike alithibitisha walipata kila walichotarajia katika mchezo wao dhidi ya Misri na aliahidi kuwa watafanya kila wawezavyo kucheza raundi ya pili ya mashindano hayo.

“Tulicheza vzuri dhidi ya Misri na kuwabana, tulifanikiwa. Lengo letu ni kuimarisha kikosi chetu kadiri tuwezavyo, “alisema gwiji huyo wa Zamalek na nyota wazamani wa Barcelona.

“Bila shaka tunacheza katika kundi ngumu, lakini tutafanya kila tuwezalo kufuzu kucheza raundi ya pili ya mashindano hayo.

“Sifikiri kama Senegal itakuwa timu dhaifu bila ya kuwa na Mane, ni mchezaji mkubwa lakini wana wachezaji wengine wakubwa katika kikosi chao, ambacho kinaweza kutwaa taji la Afcon, “alikamilisha maelezo yake.

Tanzania itaanza kampeni zake kwa kucheza mchezo wake wa kwanza katika fainali za mwaka huu za Afco baada ya kutocheza kwa miaka 39 Juni 23 kwa kucheza dhidi ya Senegal kwenye Uwanja wa Juni 30.

Wakati huohuo, nahodha wa Misri Ahmed Elmohamady alisema kuwa ushindi dhidi ya Taifa Stars ni muhimu inasaidia wachezaji, benchi la ufundi na hata mashabiki kujiamini kabla ya kuanza rasmi kwa faiali hizo za Afcon 2019.

Kocha alijaribu mifumo tofauti tofauti na kubaini baadhi ya kasoro ambazo atazifanyia kazi na kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika mashindano hayo yanayofanyika katika ardhi yao ya nyumbani.

Elmohamady ndiye aliyefunga bao pekee wakati Misri ikishinda 1-0 dhidi ya Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo.

Misri leo inacheza mchezo wa mwisho wa kirafiki dhidi ya timu ya Guinea ya Naby Keita.

Mawakala wa Tigo Pesa Wajishindia Mamilioni

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha (katikati) akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Wakala wa Pwani, Suleiman Hussein na kulia ni Vicky Ibrahim aliyejishindia sh milioni 2.5.


Na Mwandishi Wetu
ZAIDI ya mawakala 200 wa huduma ya Tigo Pesa, wamejishindia zawadi za fedha taslimu zaidi ya sh milioni 160 kwenye promosheni ya mwezi mmoja inayojulikana kama ‘Wakala Cash In Promotion’.

Promosheni hiyo ya nchi nzima iliyozinduliwa mwezi uliopita, ililenga kuwahimiza Mawakala wa Tigo Pesa nchini kufanya miamala kwa wingi ili kuweza kujishindia zawadi za fedha taslimu.

Akiwakabidhi zawadi washindi wa promosheni hiyo, kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema, kampuni ya Tigo inathamini juhudi kubwa zinazofanywa na mawakala na kuongeza kuwa promosheni hiyo ililenga kuwazadia mawakala kutokana na kazi nzuri wanayoifanya.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh milioni 3.5 Wakala wa Pwani, Suleiman Hussein wakati wa hafla ya kuwakabidhi  zawadi mawakala walioshinda. Hussein alikabidhia sh milioni 3.5  jijini Dar es Salaam.
“Kampeni hii siyo tu inaonyesha dhamira yetu ya kuwekeza kwenye biashara lakini pia adhma yetu ya kugawana tunachokipata kutokana na biashara tunayofanya pamoja na wadau wetu. Promosheni hii ni fursa nyingine ya kuwazawadia mawakala wetu fedha taslimu na bonasi  ambazo tunawaamini zitawapa moyo wa kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kuendelea kufikisha huduma jumuifu za kifedha kwa wananchi wengi zaidi,” alisema.

Kwa mujibu wa Pesha, pamoja na washindi wengine, washindi wawili wakubwa kutoka kila Kanda walipatikana ambao ni Suleiman Hussein na Vicky Ibrahim kutoka Kanda ya Pwani, Peter Myovela na Stivin Katoto kutoka Kanda ya Kusini, Anton Masawe na Athuman Mbwana kutoka Kanda ya Kaskazini pamona na Harry Lwila na Joseph Kabeba kutoka Kanda ya Ziwa.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha (kulia) akimkaabidhi Wakala wa Tigo Pesa, Vicky Ibrahim  mfano wa hundi yenye thamani ya sh milioni 2.5.
“Pamoja na washindi 2000 ambao wamejinyakulia zawadi mbali mbali za fedha taslimu kutokana na juhudi zao, tumepata washindi wengine wawili wakubwa kutoka katika kila kanda ambao kwa jumla wao ni nane, ambao wameweza kujishindia sh milioni 12 zaidi kutokana na jitihada zao. 

Tunawapongeza sana Mawakala wote ambao wamefanya vizuri na kujishindia zawadi na kwa wale ambao wahakuweza kushinda waongeze bidii ili waweze kuwa washindi katika promosheni zijazo,” alisema.

Akipokea zawadi ya sh milioni 3.5, Suleiman Hussein ambaye ni Wakala kutoka Kanda ya Pwani alisema: “Napenda kuishukuru sana kampuni ya Tigo. Promosheni hii inaonesha ni kwa kiasi gani sisi mawakala ni kiungo muhimu kwenye huduma nzima ya Tigo Pesa. Kuibuka mshindi kwenye promosheni hii ni rahisi sana kwa kuwa unahitajika kufanya kazi kwa bidii tu. Nawashauri Mawakala wenzangu wafanye kazi kwa bidi, kwani Tigo Pesa inalipa,”
Washinfi wa shindano la Mawakala wa Tigo Pewa, Suleiman Hussein (kushoto) na Vicky Ibrahim wakiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha (katikati) , baada ya kukabidhiwa mfani wa hundi katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Hussein alipata sh milioni 3.5.
Vicky Ibrahim, Wakala aliyejishindia sh milioni 2.5 alisema amefurahi kuwa mshindi wa zawadi hiyo na kuwataka wanawake kuwa mawakala wa Tigo Pesa na wale ambao tayari ni mawakala kuwekeza zaidi na kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa Tigo Pesa inalipa.
“Tigo Pesa imetuwezesha sisi wanawake kujiajiri na kuboresha maisha yetu. Nawashauri wanawake wenzangu kujiajiri au kujiongezea vipato vyao kupitia Tigo Pesa. Kwa kuwa Mawakala pia wanaweza kujishindia zawadi kupitia promoshei hii kama ambavyo mimi nilivyojishi,” alisema.

Wednesday, 12 June 2019

Kwandika Awataka TAA Kufanya Kazi Kwa Ufanisi


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
NAIBU Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa  amewakumbusha  na kuwashauri Wafanyakazi  wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuhusu ufanisi wa kazi na hatua zinazopaswa kuchukuliwa  ili Mamlaka hiyo  iweze kuongeza ufanisi wa kazi zaidi.

Akizungumza katika uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa 23 wa  Baraza la Wafanyakazi leo Jijini  Dodoma Kwandikwa alisema  Baraza lina nafasi kubwa  ya kuishauri Mamlaka juu ya maslahi bora kwa Wafanyakazi.

“Naomba  mjadili changamoto mnazokutana nazo mahala pa kazi na katika utekelezaji wa mipango ili kuhakikisha mnatoa huduma bora kwa wananchi, pia mjadili kuhusu makisio ya mapato na matumizi ya Mamlaka”alisema.

Pia alitaka  Baraza hilo lisaidie katika kuleta maelewano kazini kwani Rasilimali  watu ni muhimu katika kusimamia Rasilimali zingine na mipango katika Taasisi.

“Lazima tufanye kazi kwa umoja ili tuweze kupiga hatua, kwahiyo uwepo wenu ni muhimu  katika kujadiliana namna ya kuendeleza Taasisi kwa kushirikiana”alisema.
 
Pia Kwandikwa alisema Baraza liweke mazingira ya kuongeza tija kwa Watumishi wanaotimiza majukumu yao ambapo lengo ni kutambua mchango wao na kuuthamini.

“Watumishi pia watimize majukumu yao kwa weledi kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu za Utumishi wa umma”alisema.

Katika hatua nyingine Kwandikwa amewataka wafanyakazi wa Mamlaka  wafanye  maandalizi juu ya ufunguzi wa Jengo la tatu la abiria.

“Endeleeni kufanya uchunguzi juu ya vihatarishi vinavyoweza kujitokeza baada ya kuanza matumizi ya jengo hilo,na  mshirikishane na kudhibiti mapema vihatarishi hivyo”alisema.

Pia aliwataka Watumishi sekta ya Anga kufanya kazi kwa weledi ili kuboresha huduma za usafiri wa Anga ili kuongeza ushindani wa Kitaifa na Kimataifa.

Pia alisisitiza kuwa ni  muhimu  Watumishi wa Mamlaka kujitambua kuwa  wanamchango katika kukuza pato la Taifa kutokana na huduma wanazotoa ambazo  zina  mchango Mkubwa katika ujenzi wa Taifa.

Awali, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Mhandisi Julius Ndyamukama kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi aliainisha baadhi ya changamoto zinazoitatiza Taasisi kuwa ni maslahi duni kwa Wafanyakazi, uchache wa Wafanyakazi pamoja na nyenzo za ufanyaji kazi kama magari ya Zimamoto.

Ambapo Kwandikwa alisema “Serikali itafanyia kazi changamoto hizo ili kuhakikisha inaboresha sekta ya Usafiri wa Anga huku akitoa wa wito kufanya kazi kwa bidii na  weledi mkubwa huku akisisitiza Maazimio ya Baraza hilo yale ambayo yamekuwa changamoto yawe fursa ili yaweze kufanyiwa kazi.

Mkutano huo wa 23 wa Baraza kuu la Wafanyakazi unafanyika kwa kwa siku mbili katika ukumbi wa Takwimu Jijini hapa.