Saturday 15 June 2019

Mawakala wa Tigo Pesa Wajishindia Mamilioni

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha (katikati) akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Wakala wa Pwani, Suleiman Hussein na kulia ni Vicky Ibrahim aliyejishindia sh milioni 2.5.


Na Mwandishi Wetu
ZAIDI ya mawakala 200 wa huduma ya Tigo Pesa, wamejishindia zawadi za fedha taslimu zaidi ya sh milioni 160 kwenye promosheni ya mwezi mmoja inayojulikana kama ‘Wakala Cash In Promotion’.

Promosheni hiyo ya nchi nzima iliyozinduliwa mwezi uliopita, ililenga kuwahimiza Mawakala wa Tigo Pesa nchini kufanya miamala kwa wingi ili kuweza kujishindia zawadi za fedha taslimu.

Akiwakabidhi zawadi washindi wa promosheni hiyo, kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema, kampuni ya Tigo inathamini juhudi kubwa zinazofanywa na mawakala na kuongeza kuwa promosheni hiyo ililenga kuwazadia mawakala kutokana na kazi nzuri wanayoifanya.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh milioni 3.5 Wakala wa Pwani, Suleiman Hussein wakati wa hafla ya kuwakabidhi  zawadi mawakala walioshinda. Hussein alikabidhia sh milioni 3.5  jijini Dar es Salaam.
“Kampeni hii siyo tu inaonyesha dhamira yetu ya kuwekeza kwenye biashara lakini pia adhma yetu ya kugawana tunachokipata kutokana na biashara tunayofanya pamoja na wadau wetu. Promosheni hii ni fursa nyingine ya kuwazawadia mawakala wetu fedha taslimu na bonasi  ambazo tunawaamini zitawapa moyo wa kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kuendelea kufikisha huduma jumuifu za kifedha kwa wananchi wengi zaidi,” alisema.

Kwa mujibu wa Pesha, pamoja na washindi wengine, washindi wawili wakubwa kutoka kila Kanda walipatikana ambao ni Suleiman Hussein na Vicky Ibrahim kutoka Kanda ya Pwani, Peter Myovela na Stivin Katoto kutoka Kanda ya Kusini, Anton Masawe na Athuman Mbwana kutoka Kanda ya Kaskazini pamona na Harry Lwila na Joseph Kabeba kutoka Kanda ya Ziwa.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha (kulia) akimkaabidhi Wakala wa Tigo Pesa, Vicky Ibrahim  mfano wa hundi yenye thamani ya sh milioni 2.5.
“Pamoja na washindi 2000 ambao wamejinyakulia zawadi mbali mbali za fedha taslimu kutokana na juhudi zao, tumepata washindi wengine wawili wakubwa kutoka katika kila kanda ambao kwa jumla wao ni nane, ambao wameweza kujishindia sh milioni 12 zaidi kutokana na jitihada zao. 

Tunawapongeza sana Mawakala wote ambao wamefanya vizuri na kujishindia zawadi na kwa wale ambao wahakuweza kushinda waongeze bidii ili waweze kuwa washindi katika promosheni zijazo,” alisema.

Akipokea zawadi ya sh milioni 3.5, Suleiman Hussein ambaye ni Wakala kutoka Kanda ya Pwani alisema: “Napenda kuishukuru sana kampuni ya Tigo. Promosheni hii inaonesha ni kwa kiasi gani sisi mawakala ni kiungo muhimu kwenye huduma nzima ya Tigo Pesa. Kuibuka mshindi kwenye promosheni hii ni rahisi sana kwa kuwa unahitajika kufanya kazi kwa bidii tu. Nawashauri Mawakala wenzangu wafanye kazi kwa bidi, kwani Tigo Pesa inalipa,”
Washinfi wa shindano la Mawakala wa Tigo Pewa, Suleiman Hussein (kushoto) na Vicky Ibrahim wakiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha (katikati) , baada ya kukabidhiwa mfani wa hundi katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Hussein alipata sh milioni 3.5.
Vicky Ibrahim, Wakala aliyejishindia sh milioni 2.5 alisema amefurahi kuwa mshindi wa zawadi hiyo na kuwataka wanawake kuwa mawakala wa Tigo Pesa na wale ambao tayari ni mawakala kuwekeza zaidi na kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa Tigo Pesa inalipa.
“Tigo Pesa imetuwezesha sisi wanawake kujiajiri na kuboresha maisha yetu. Nawashauri wanawake wenzangu kujiajiri au kujiongezea vipato vyao kupitia Tigo Pesa. Kwa kuwa Mawakala pia wanaweza kujishindia zawadi kupitia promoshei hii kama ambavyo mimi nilivyojishi,” alisema.

No comments:

Post a Comment