Saturday, 4 March 2017

Yanga mikononi mwa Mtibwa sugar kesho kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro ikishinda kuiondoa Simba kileleni Ligi Kuu BaraNa Mwandishi Wetu
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, kesho wana nafasi nyingine yakuiondoa kileleni Simba wakati watakapocheza dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Yanga endapo watashinda mchezo huo watafikisha pointi 55 sawa na Simba lakini watakuwa na faida ya mabao mengi ukilinganisha na watani zao hao.

Kimabao Yanga ina mabao ya kufunga 49 na kufungwa 11 wakati Simba wakifunga mabao 38 na kufungwa mabao nane tu, hivyo Yanga watakuwa na mabao mengi yatakayowawezesha kurudi kileleni.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema kuwa, akili zao wamezielekeza katika mchezo huo wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Alisema timu yao inajua umuhimu wa mchezo huo wa leo na ndio maana mambo yote wameyaweka kando na kuelekeza mawazo yao katika mchezo huo.

Mtibwa Sugar ni moja ya timu sumbufu hasa inapocheza mbele ya mashabiki wao kwenye Uwanja wa Jamhuri pamoja na ule wa Manungu.

No comments:

Post a Comment