Thursday, 9 March 2017

Wanawake Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) walivyosheherekea Siku yao duniani kimkoa ilifanyika Mwembe Yanga


Wanawake wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)  wakiungana na mamia ya wanawake wengine duniani, kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani, iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.

Siku ya Wanawake Duniani iliadhimishwa jana kwenye viwanja vya Mwem be Yanga Jijini Dar es Salaam, ambapo wanawake kutoka Ofisi za serikali na binafsi waliungana na wenzao kusherehekea siku hiyo muhimu. Pichani ni wanawake kutoka Idara mbalimbali za Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakifurahia siku hiyo.
Wanawake kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakiserebuka kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam, wakiifurahia siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa jana, ambapo mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva  aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Wanawake wakiwa kwenye furaha wakiadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, iliyoadhimishwa jana katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam, ikiwa na kauli mbiu ya Tanzania ya Viwanda; Wanawake ni Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi. 

No comments:

Post a Comment