Saturday 4 March 2017

Matukio mbalimbali katika picha Uwanja wa Ndenge wa Bukoba unavyofanya kazi

Baadhi  ya madarasa ya shule ya msingi Tumaini iliyopo Kata ya Kashai, wilaya ya Bukoba Mjini  yakisubiri kuhamishwa kutokana na usalama baada ya kuwa karibu na eneo la Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
Baadhi ya majengo mapya ya madarasa ya shule mpya ya msingi ya Tumaini, yaliyopo mtaa wa Mafumbo, Kata ya Kashai yakiwa kwenye hatua ya mwisho ya ujenzi wake. Shule  hiyo  ina madarasa 24 ya kuanzia darasa la kwanza hadi la Saba, na madarasa matatu kati ya hayo ni ya watoto wenye mahitaji maalumu.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Rwambaizi ya Karagwe  mkoani Kagera wakiwa  kwenye kiwanja cha ndege cha Bukoba, katika ziara ya kimafunzo juzi.
Abiria wakiwasilisha taarifa zao  pamoja na ukaguzi wa tiketi, kabla ya kupanda ndege ya Auric  wakitokea kwenye kiwanja cha ndege cha Bukoba  kwenda Mwanza.
Msimamizi wa Kitengo cha Usalama, Bi. Theodora Myaka wa Kiwanja cha ndege cha Bukoba (kushoto) akimkagua abiria Bi. Jasmindee Dhaliwa, Raia wa Bulgaria huku Ofisa Usalama Msaidizi, Reginald Baraka akishuhudia.

No comments:

Post a Comment