Na Bahati Mollel-TAA, Iringa
TIMU
za soka za Uchukuzi na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) zilizopo kundi ‘A’
na ‘B’ zinakaribia kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mei Mosi baada
ya leo kushinda michezo ya iliyofanyika kwenye uwanja wa Samora, ambapo kila
mmoja zinaongoza kundi lake kwa kujikusanyia pointi sita.
Uchukuzi
inafuatiwa na mabingwa watetezi Geita Gold Mine (GGM) wenye pointi mbili, NAO
na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yenye pointi moja kila mmoja; wakati
Tanesco inafuatiwa na Tumbaku nayo inapointi sita lakini imezidiwa magoli ya
kufunga, huku RAS Iringa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakiwa hawana
pointi.
Katika
mechi hizo za jana Uchukuzi waliwafunga Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu
(NAO) kwa magoli 3-1. Nao ndio walikuwa wa kwanza kupachika bao katika dakika
ya 45 kupitia kwa Peter Dihoko aliyeunganisha kona ya George Mlelwa.
Uchukuzi
walisawazisha katika dakika ya 60 kupitia wa Kado Nyoni, huku bao la pili
lilifungwa na Omary Kitambo dakika ya 63 na bao la tatu dakika ya 68
lililofungwa na Issack Ibrahim.
Mfungaji Ester Turuka (GA-orange
katikati) wa RAS Iringa akijaribu kuwania mpira na Cecy Kanza (WD) Tanesco
katika mchezo wa michuano ya Mei Mosi uliofanyika leo kwenye uwanja wa Chuo
Kikuu cha Katoliki Iringa (RUCU). RAS Iringa walishinda kwa magoli 27-14 (Picha
na Bahati Mollel wa TAA).
Nao
Tanesco waliwachapa RAS Iringa kwa magoli 4-0, ambapo matatu yaliyofungwa na
Kurwa Mangara katika dakika ya 19, 34 na 59 huku Salehe Bakari alifunga bao la
nne dakika ya 66.
Katika
mchezo wa netiboli timu ya RAS Iringa iliwafunga Tanesco kwa magoli 27-14.
Washindi walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 9-7. Nayo Ikulu walipewa
ushindi wa mezani wa magoki 40 na pointi mbili baada ya Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro (NCAA) kushindwa kufika uwanjani Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCU) kwa
kuwa na majeruhi wengi waliotokana na kuvuta kamba.
Daktari wa timu ya Uchukuzi, Hawa Senkoro
(kushoto) akimchua misuli mchezaji wake Kassim Sabu aliyebanwa na misuli katika
mchezo wa soka wa michuano ya Kombe la Mei Mosi dhidi ya Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi wa Hesabu (NAO) uliofanyika leo kwenye uwanja wa Samora, ambapo
Uchukuzi walishinda kwa magoli 3-1. (Picha na Bahati Mollel wa TAA).
Katika
mchezo wa kuvuta kamba kwa wanawake timu ya Uchukuzi ilivutwa na RAS Iringa 1-0
baada ya mvuto wa awali kutoka sare;
huku kwa upande wa wanaume wa Uchukuzi waliwavuta Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi wa Hesabu (NAO) kwa mivuto 2-0.
Michezo
mingine ya kamba wanawake walivutwa na MUHAS mivuto 2-0; nayo NAO waliwavuta
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mvuto 1-0 kwa upande wa wanaume.
Mlinzi Jacky Sanga (mwenye mpira) wa
Tanesco akitafuta wa kumrushia katika mchezo wa michuano ya Kombe la Mei Mosi
kwa mchezo wa netiboli dhidi ya RAS Iringa uliofanyika leo kwenye uwanja wa Chuo
Kikuu cha Katoliki Iringa (RUCU). (Picha na Bahati Mollel wa TAA).
Michuano hiyo inaendelea kesho kwa upande wa netiboli wakati timu ya Uchukuzi itacheza na RAS Iringa Uwanja wa RUCU; huku katika soka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wataumana na Tumbaku ya Morogoro, na GGM watacheza na Uchukuzi kwenye Uwanja wa Samora; wakati katika kamba RAS Iringa kuumana na Tanesco kwa wanawake.
No comments:
Post a Comment