ROME, Italia
HAKUNA aliyetarajia Barcelona inaweza kutolewa na AS
Roma katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya baada ya vinara hao wa La
Liga kuwa mbele kwa mabao 4-1 baada ya kushinda katika mchezo wa kwanza.
Hata hivyo, Barcelona imefungishwa virago baada ya
kupokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Roma katika mchezo ambao wenyeji ndio
walikuwa wenyeji. Roma imesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini.
Kiungo wa Barca Andres Iniesta alikuwa hataki
kukubali kama timu yake imepokea kichapo hicho, ambacho kimeitoa katika mbio za
kuwania taji la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Wakati Iniesta akishindwa kuamini kilichotokea kwa
timu yake, mchezaji mwenzake wa timu hiyo, Sergio Busquets amekiita kipigo
hicho kuwa ni kibaya zaidi katika historia yake ya soka.
Awali, safari ya Barca kucheza nusu fainali
ilionekana kuiva wakati timu hiyo ilipouanza mchezo huku ikiwa na faida ya
mabao 4-1, lakini walionesha kiwango kibovu kabisa msimu huu, katika mchezo huo
uliofanyika kwenye Uwanja wa Olimpiki.
Baracelona imetupwa nje kwa mabao ya AS Roma
yaliyofungwa na Edin Dzeko, Daniele De Rossi kwa penalti na na lile la kichwa
lililopachikwa na Kostas Manolas header.
"Inauma kwasababu hakuna mtu aliyetarajia
kichapo hiki baada ya kuwa na faida ya mabao manne tuliyopata kutoka katika
mhezo wa kwanza, lakini hilo ndilo linakufanya kutambua maana ya michuano ya
Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, “alisema.
Kufungwa huko kwa Barcelona kumeshuhudia timu hiyo
ikitolewa katika hatua ya robo fainali ya mashindano hayo kwa mara ya tatu
mfululizo na kukatisha ndoto zao za kushinda mataji matatu msimu mmoja.
"Ni ngumu kukubali kutolewa huku kwasababu
tulikuwa na matumaini kibao msimu huu na kwa mara nyingine tena (Ligi ya
Mabingwa) imetuacha solemba, “aliongeza kiungo huyo.
"Inasikitisha sana baada ya kuwa na msimu mzuri.
Sasa tumepata pigo.”
Nahodha huyo wa Barca alibainisha kuwa huenda
mwishoni mwa msimu huu akaondoka katika klabuhiyo aliyoitumikia kwa muda mrefu
na kwenda China kucheza soka, ambako ataufurahisha moyo wake.
"Ni usiku mzito, huzuni na tunatakiwa kuomba
radhi kwa mashabiki wetu kwa jisi tulivyoangua, “alisema.
"Hli ni pigo kubwa ambalo nimewahi kulipa katika
kipindi chote nilichokuwa Barcelona kwasababu jinsi kilivyotokea.”
Barcelona, ambao ni mabingwa mara tano pia walifungwa
3-0 katika hatua kama hiyo ya robo fainali msimu uliopita walipocheza dhidi ya
Juventus.
"Nitakuwa muongo kama nitasema kuwa eti
tutatumia kipigo hicho kama somo kwasababu mwaka jana tulitolea kwa njia kama
hii hii, “aliongeza Busquets.
"Matokeo yetu Ulaya katika miaka miwili
iliyopita yamekuwa mabaya sana, kama tunataka kushinda Ligi ya Mabingwa wa
Ulaya, basi tunatakiwa kubadilika kabisa.”
No comments:
Post a Comment