MANCHESTER, Liverpool
KOCHA wa Liverpool Jurgen Klopp ameimwagia sifa timu
yake baada ya kupenya na kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya
baada ya kuifunga tena Manchester City kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa
kwenye Uwanja wa Etuhad.
Kwa matokeo hayo, Liverpool imesonga mbele kwa ushindi
wa jumlaya mabao 5-1, kufuatia ushindi wa timu hiyo katika mchezo wao wa kwanza
wa mabao 3-0.
"Tumefunga mabao matano dhidi ya Man City na
tumeruhusu kufungwa bao moja tu. Kwa kweli idadi kama hii ya mabao haiwezekani
kirahisi, “alisema kocha huyo Mjerumani.
"Vijana walipata soluhisho katika kipindi cha
pili. Tayari katika kipindi cha kwanza ulikuwa na nafasi mbili au tatu hivi,
hivyo ilikuwa rahisi kwangu na vijana kuona muendelezo wa mchezo. Tukafanikiwa
kupata mabao.”
Bao la mapema la Gabriel Jesus liliwapa matumaini
Manchester City kama wanaweza kupindua matokeo ya awali na kuibuka na ushindi
mnono, ambao ungewapeleka katika nusu fainali, lakini hilo halikufanikiwa.
Badala yake, bao la Mohamed Salah katika dakika ya 39
liliiweka Liverpool kukontroo mpira kabla Roberto Firmino hajakamilisha na
kuiwezesha Liverpool kutinga kwa maraya kwanza nusu fainali katika kipindi cha
muongo mmoja.
Liverpool kwa mara ya mwisho ilicheza fainali ya Ligi ya Mabigwa wa Ulaya katika msimu wa mwaka 2007-08 na ni matumainiyake sasa yameongezeka baada ya kutolewa kwaBarcelona.
Vigogo hao wa Hispania walitolewa baada ya kufungwa
3-0 na AS Roma, huku Roma ambayo ni timu ya zamani ya Salah imesonga mbele kwa
bao la ugenini kufuatia sare ya jumla ya mabao 4-4.
Klopp alisema kutolewa kwa Barcelona: "Kumeinua
ari kwa timu zilizobaki.
"Sio kuidharau AS Roma. Walimpoteza Salah na
sasa wako katika nusu fainali. Hicho ni kitu kingine.
"Mashindano haya yametenda haki na nilitarajia
fainali ya kawaida kabisa kati ya Manchester City dhidi ya Barcelona, na sasa
wote wametolewa.
"Lakini sasa kutakuwa na timu mbili zenye nguvu
pamoja na kuongeza AS Roma na sisi. Tutaona nini kitatokea lakini na hicho sio
kitu cha mimi kufikiria.”
Kocha wa Man City, Pep Guardiola aliwataka wachezaji
wake kurejea kiakili katika hali ya kawaida baada ya kuwa na wiki mbaya ya
msimu baadaya kutolewa kwa mara ya tatu mfululizo.
Man City ilipata pigo jingine mwishoni mwa wiki
iliyopita baada ya kushuindwa kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu baada ya kufungwa
na majirani zao wa Manchester United.
City ina pointi 13 kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu
ya England na kilichobaki ni muda tu kabla timu hiyo haijavikwa taji la
England.
Guardiola anataka wachezaji wake kufanya kweli katika
mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Tottenham utakaofanyika Wembley Jumamosi ili
kutangaza ubingwa endapo watashinda.
"Sasa tunatakiwa kwenda Tottenham tukiwa
tumebadilika kifikra, “alisema kocha huyo Mhispania.
"Kipindi cha kwanza tulifanya kila kitu, lakini
cha pili tulichemsha.”
Guardiola alisema City waliathirika pia na maamuzi
mabovu walipocheza dhidi ya Liverpool.
Leroy Sane alifunga na lingefanya matokeo kuwa 2-0
kama sio mwamuzi kulikataa bao hilo, ambapo Guardiola alililalamikia hadi
kutolewa uwanjani.
No comments:
Post a Comment