LONDON, England
KOCHA wa Manchester United Jose Mourinho ameongeza
mkataba utakaomuweka katika klabu hiyo hadi mwaka 2020, ukiwa na nafasi ya
kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Mkataba wa awali wa kocha huyo mwenye miaka 54 Old
Trafford unatakiwa kumalizika mwaka 2019.
Mourinho alisema “amefurahi” kuwa Man United
“wananiamini kuwa kocha sahihi kwa ajili ya klabu kubwa….”
"Najihisi mtu mwenye bahati kufanya kazi na
kundi la vijana wa ajabu, “aliongeza.
"Mkataba wangu wa awali ulikuwa ni wa miaka
mitatu, sasa tumefanya uamuzi wa wazi kwa kila mmoja sio miaka mitatu, ni minne
au mitano, nani anajua, zaidi.”
Mourinho, aliteuliwa kuwa kocha wa Man United
kuchukua nafasi ya Louis van Gaal Mei mwaka 2016, ambapo alishinda Kombe la EFL
na lile la Ligi ya Ulaya katika msimu wake wa kwanza.
Msimu huu Man United wako katika nafasi ya pili
katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, wakiwa nyuma ya Manchester City, huku
timu hiyo ikiwa bado iko katika mbio za Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA.
"Tumeweka viwango vya juu, tukishinda mataji matatu
katika msimu mmoja, lakini hicho ni kiwango nilichotarajia, “alisema kocha huyo
Mreno.
Woodward alimpongeza Mourinho kwa kazi yake nzuri na
weledi”, wakati akitimiza lengo la klabu kukuza vipaji vya wachezaji chipukizi
na wenye viwango”.
Akizungumza mapema juzi katika mkutano na waandishi
wa habari, kabla ya kuingia mkataba huo mpya, Mourinho aliipongeza klabuhiyo
kwa kumsajili Alexis Sanchez kutoka Arsenal.
Alisema mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile amejiunga
kutoka klabu ya ajabu na kwenda katika klabu kubwa huku ikishuhudia kiungo wa
Armenia Henrikh Mkhitaryan akitua upande mwingine.
Mourinho alisema ni usajili mkubwa kwa kila mtu na
kuthibitisha Sanchez atakuwa katika kikosi cha United kilichotarajia kucheza
Kombe la FA jana dhidi ya Yeovil.
No comments:
Post a Comment