Na Mwandishi Wetu
TANZANIA imepanda kwa nafasi tisa katika Viwango vya
ubora wa soka Ulimwenguni vilivyotolewa na Shirikisho la Kimataifa la Soka, FIFA, mapema leo.
Awali, Tanzania ilikuwa inashika nafasi ya 146 na
sasa inashika nafasi ya 137 baada ya kukusanya jumla ya pointi 223 kutoka alama
186 ilizopata mwezi uliopita.
Kupanda kwa Tanzania kunatokana na kucheza michezo
miwili ya kirafiki ya kimataifa katika kalenda ya FIFA, ambapo ilicheza na
Algeria na kufungwa mabao 4-1 na kuifunga DR Congo kwa mabao 2-0.
Katika Ukanda wa Afrika Mashariki, Uganda imeendelea
kushika usukani ikiwa katika nafasi ya 74, Kenya nafasi ya 113, Rwanda nafasi
ya 123, Sudan ya 126 na Sudan Kusini inashika nafasi ya 155.
Kwa upande wa Afrika, Tunisia inaongoza ikiwa nafasi
ya 14 duniani baada ya kupanda kwa nafasi tisa wakifuatiwa na Senegal iliyopo katika nafasi ya 28 na DR Congo wapo
nafasi ya 38.
Ujerumani inaongoza ikifuatiwa na Brazil, Ubelgiji
nafasi ya nne ipo Ureno na Argentina inakamilisha tano bora za FIFA.
No comments:
Post a Comment