Emmanuel Okwi akishangilia baada ya kunga bao wakati Simba ilipocheza dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jahmuri mjini Morogoro leo. |
Na Mwandishi Wetu
VINARA wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba wamezidi
kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, baada ya jana kuifunga Mtibwa Sugar
kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa.
Kwa ushindi huo, Simba sasa imefikisha pointi 52
baada ya kushuka dimbani mara 22 ikimuacha mtani wake Yanga akiendelea kuwa
katika nafasi ya pili kwa pointi 46, lakini akiwa na mchezo mkononi.
Yanga wenyewe wanacheza kesho dhidi ya Singida United
katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Simba waliiuanza mchezo huo kwa kufanya mashmbulizi
ya mara kwa mara ndani ya dakika 15 za mchezo huo kupitia washambuliaji wake
Emmanuel Okwi, Shiza Kichuya na John Bocco na kuleta msukosuko, langoni mwa
Mtibwa Sugar .
Katika mchezo huo, ``Simba iliandika bao la
kuongoza katika dakika ya 23 lililofungwa na Emmanuel Okwi kufuatia krosi ya
Kichuya aliyepiga krosi iliyomkura John Bocco aliyetoa pasi ya kichwa kwa Okwi aliyeukwamisha
mpira kirahisi wavuni.
Dakika ya 37 Mtibwa walipata kona mbili mfululizo,
lakini zote hazikuzaa matunda na hizo zilitokana na timu hiyo kufanya
mashambulizi ya nguvu langoni mwa wapinzani wao.
Hata hivyo vijana wa Simba waliimarika zaidi kipindi
cha kwanza, licha ya mvua kunyesha katika kipindi hicho, ambapo Bocco na Okwi walikuwa wakibadilisha
nafasi kucheza kipindi hicho cha kwanza.
Azam FC ambao walicheza juzi na kutoka suluhu Mbeya
City na hivyo kendelea kuchechemea katika nafasi ya tatu akiwa na pointi 45
lakin akiwa amecheza mchezo mmoja zaidi.
Simba mchezo unaofuata itacheza dhidi ya Mbeya City mwishoni
mwa wiki katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment