LONDON, England
KOCHA Arsene Wenger amejikuta lawamani baada ya Arsenal
kutolewa katika raundi ya tatu ya Kombe la FA na timu ya daraja la kwanza ya Nottingham
Forest.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa City
Ground, Arsenal ilijikuta ikipokea kichapo cha mabao 4-2 kutoka kwa timu hiyo
ya daraja la kwanza.
Wenyeji Nottingham Forest walipata bao la kwanza wakati
Eric Lichaj alipofunga kwa kichwa bao la kuongoza kwa mpira wa karibu wa
kichwa.
Hatahivyo, furaha za bao hilo zilidumu kwa dakika tatu tu
wakati Per Mertesacker alipofunga bao la kusawazisha katika dakika ya 23 baada
ya mpira wa kichwa wa Rob Holding kugonga mwamba.
Lichaj alifunga tena bao la kungoza kwa Forest, ambayo
inaongozwa na kocha Gary Brazil,
ambapo beki huy Mmarekani alifunga ndami ya
boksi dakika moja kabla ya mapumziko.
Katia kipindi cha pili, Forest iliongeza kasi wakati Ben
Brereton alipompeleka sokoni kipa David Ospina na mpira kujaa wavuni.
Danny Welbeck alipunguza kipigo kwa timu ya Wenger ambayo
iliundwa na wachezaji wengi wasio wa kikosi cha kwanza baada ya kipa wa Forest
Jordan Smith kuhindwa kuzuia shuti hilo.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa Arsenal kutolewa katika raundi
ya tatu ya Kombe la FA tangu Januari mwaka 1996 waliporudiana na Sheffield
United.
Penalti ilizidi kumchefua Wenger, ambaye hivi karibuni
alifungiwa na Chama cha Soka (FA) kwa kosa la kuwalalamikia waamuzi.
Katika mchezo huo, Wenger alishuhudia mchezo huo kutokea
jukwaani baada ya kufungiwa mechi tatu kukaa katika benchi la timu yake.
No comments:
Post a Comment