Na Mwandishi Wetu
MBIO za Ngorongoro Marahon zenye lengo la Kukimbiza
Jangili, ambazo mwaka huu zitafanyika Aprili 21 zimefikia katika hatua nzuri.
Kauli Mbiu yam bio hizo mwaka huu ni `Kukimbiza
Jangili’, ambapo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCCA) ndio mdhamini mkuu
ikisaidia na Bonite Bottlers ya mjini Moshi, ambayo hutengeneza maji ya
Kilimanjaro na soda jamii ya Coca Cola.
Tayari wanariadha zaidi ya 200 wamejisajili kwa ajili
ya kushiriki mbio hizo, ambazo waandaaji wanasema kuwa mwaka huu zitakuwa na
msisimko mkubwa katika maeneo tofauti tofauti.
WAANDAAJI
WANENA
Mkurugenzi wa mbio hizo, Meta Petro akizungumza na
gazeti hili anasema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na ni matarajio yao
makubwa kuwa mwaka huu msisimko utakuwa mkubwa zaidi tofauti na mwaka jana.
Alisema kuwa ni mataraji yao kuwa mwaka hadi mwaka
mashindano hayo yatakuwa yakibadilika na kushirikisha washiriki kibao kutoka
ndani na nje ya nchi.
Petro ambaye ni mwanariadha wazamani wa kimataifa wa
Tanzania, anasema kuwa wakimbiaji nyota karibu wote nchini wamethibitisha
kushiriki mbio hizo, ambazo huanzia katika lango kuu la kuingilia na kutokea
katika Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.
Anasema kuwa hivi karibuni watamtangaza mgeni rasmi
wa mbio hizo, ambazo mbali na kupiga vita ujangili wa wanyama pori, pia
zinatumika kuinua vipaji vya wanariadha nchini wa rika tofauti tofauti.
KUONGEZWA
ZAWADI
Anasema kuwa ili kuongeza msisimko na ushindano wa
mbio hizo wameandaa zawadi, ambapo sasa washindi wengi watazawadi tofauti na
huko nyuma, ambapo watu wachache wa kwanza ndio walizawadiwa.
Alisema kuwa baada ya kutafakari sasa washindi wengi
wa mbio za kilometa 21 watapata zawadi ili kuongeza ushindani na kuvuta
washiriki wengi.
Mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha Sh milioni
1 huku wa pili Sh 500,000 wakati yule watatu atapata Sh 250,000, ambapo zawadi
zitatolewa hadi kwa mwanariadha wa 10 bora.
Huku kwa watoto wadogo, ambao watashiriki mbio za
kilometa 2.5 zawadi zitatolewa hadi tano bora wakati huko nyuma walikuwa
wakipata zawadi washindi watatu tu wa kwanza.
Kingine kikubwa katika mbio nyingi washindi wa
kilometa tano hawapati zawadi, lakini Ngorongoro Marathon hutoa kifuta jasho
kwa washindi wa mbio hizo, ambazo huitwa za kujifurahisha.
ADA
ZA USHIRIKI
Kwa washiriki wakilometa 21 kila mshiriki atatakiwa
kulipia Sh 10,000 kwa Raia wa Watanzania wakati raia wakigeni akila mmoja
atalipa mkiasi cha dola za Marekani 50 wakati watoto watakimbia bure.
Wale watakaoshiriki mbio za kilometa tano watalipia
kiasi cha Sh 10,000 kwa watanzania wakati wagemi watalipa dola 10 na timu,
yaani kampuni kama itapeleka wafanyakazi wake kushiriki, basi itatakiwa kulipia
dola za Marekani 500.
MBIO
ZA MWAKA HUU
Wanyama kama tembo, kifaru wamekuwa wakiuawa na
majangili kwa ajili ya meno yao wakati twiga na pundamilia wanauawa kwa ajili
ya nyama zao huku simba na chui wanapata majanga kutokana na ngozi zao, hivyo
mbio za mwaka huu zinaendeleza kampeni ya kupiga vita ujangili huo.
Waandaaji wameamua kupambana na ujangili huo ili
kuwaepusha wanayama hao na janga la kuawa kwani wakimalizika, taifa litakosa
fedha za kigeni kupitia katika utalii wa kuangalia wanyama.
Mbio hizo zilianza tangu mwaka 2008 na lengo likiwa
ni kupiga vita tatizo la taifa na dunia la kuuawa ovyo wanyama kwa ajili ya
pembe na ngozi zao.
Huko nyuma lengo lilikuwa kupiga vita malaria katika
eneo la Karatu na vitongioji vyakle pamoja na gonjwa hatari la ukimwi, lakini
baada ya kupungua kwa tatizo hilo,
Wamekua wakipiga vita ujangili, ambao
umekithiri katika mbuga zetu hapa nchini.
Mbio hizo mwaka huu zinatimiza miaka 11 tangu
kuanzishwa kwake na zimekuwa zikiandalia kwa umakini mkubwa chini ya Petro
pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi, Filbert Bayi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa
Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).
No comments:
Post a Comment