Baadhi ya wachezaji wa timu ya Uchukuzi
wakiwa na vikombe vyao 13 walivyoshinda kwenye mashindano ya Kombe la Mei Mosi
yaliyomalizika jana mkoani Iringa. (Picha Zote na Bahati Mollel wa TAA).
Na
Bahati Mollel-TAA, Iringa
MWENYEKITI wa Tuico Taifa, Paulo Sangeze amesikitishwa na mahudhurio duni yaliyosababishwa na wanamichezo wafanyakazi kunyimwa fursa kushiriki Michezo ya Mei Mosi mwaka huu iliyofanyika mjini hapa.
Alisema kuwa anaungana na waandaaji kushangaa idadi ndogo ya ushiriki katika mashindano ya mwaka huu.
“Mashirikisho yote ya wafanyakazi tumesikitika kwa idadi hii ndogo na tutahakikisha miaka ijayo timu zinaongezeka zaidi, na tunaipongeza timu ya netiboli ya Ofisi ya Rais Ikulu kushiriki wameonesha mfano mzuri,” amesema Bw. Sangeze.
Pia amesema michezo mahala pa kazi inasaidia kujenga miili ya wafanyakazi na kuongeza tija na bidii kazini, kwani viongozi wasiopenda michezo wanasababisha wafanyakazi kupata magonjwa nyemelezi.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Mei Mosi, Bi. Joyce Benjamin alisema Rais John Pombe Magufuli hajawahi kukataza michezo, na inashangaza utashi wa viongozi wasiopenda michezo wanaokataza timu zao kushiriki kwenye michezo.
“Tunaomba viongozi wa vyama vya wafanyakazi wa kila eneo la kazi kuingilia kati juu ya hili katika dhana nzima ya wafanyakazi kufanya michezo na kushiriki kwenye michezo ya mashirikisho mbalimbali kama Shimiwi, Shimuuta na kutofanya michezo kunapingana na ilani ya Chama cha Mapinduzi, inayosema wazi juu ya kuinua michezo nchini,” amesema Bi. Benjamin.
Katika mashindano hayo, klabu ya michezo ya Uchukuzi iliyopo (Sekta ya Uchukuzi) imebuka kidedea katika
michezo ya michuano ya Kombe la Mei Mosi 2018 baada ya kushinda vikombe 13 vya
michezo 10 iliyoshindaniwa kwenye viwanja mbalimbali mjini hapa.
Bi. Sharifa Amir wa Uchukuzi (kulia) akikabidhiwa kombe la ushindi wa kwanza wa mchezo wa draft kwa wanawake kutoka kwa mgeni rasmi Bw. Paul Sangeze ambaye ni Mwenyekiti wa TUICO Taifa. |
Timu
hiyo inayoundwa na wachezaji mahiri imeweza kutwaa ubingwa wa kwanza kwa
wanaume katika michezo ya mbio za baiskeli (Chaptele Muhumba), draft (Johanson
Ngido), bao (Said Omar) na kuvuta kamba, huku kwa wanawake wametwaa ubingwa
katika mbio za baiskeli na riadha (Scolastica Hasiri), bao (Sharifa Amir) na
draft olnel) na karata wanawake na wanaume (Zamatradi Yusufu na Mosses
Machunda).
Timu
ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) imeshika nafasi ya pili kwa kujikusanyia
vikombe tisa kwa kutwa ubingwa wa soka, riadha wanaume (Lazaro Lugano) huku
ushindi wa pili katika michezo ya riadha wanawake (Cartace Manampo), na
baiskeli (Happy Mwanga), karata (Sheila Mwihava) na Nkwabi Kadago (mwanaume),
na ushindi wa tatu netiboli, Stanley Umbe (baiskeli) na Jackline Massawe (bao).
Timu
ya Chuo Kikuu cha Tiba ya Sayansi (MUHAS) wamekuwa watatu kwa kujikusanyia
vikombe vitano vya bingwa wa karata wanawake (Emily Kyando), ; mshindi wa pili
katika bao (Severina Mnyaga), huku mshindi wa tatu michezo ya kuvuta kamba na
baiskeli wanawake (Severina Mnyaga) na dratf (Rebecca Chaula).
Timu
ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wameshika nafasi ya nne kwa kujikusanyia vikombe
vinne vya ushindi wa pili katika riadha, baiskeli na bao wanaume (Michael Luanga), Nehemiua Johnas na Suleiman Chitanda, huku
nafasi ya tatu ya draft ilichukuliwa na Joseph Mlimi.
Timu
ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NAOT) wamejikusanyia vikombe vitatu
pekee na kuwa watatu. Vikombe vya ushindi wa pili draft wanawake na wanaume
Rosemary Skainde na Alphonce Sika na ushindi wa tatu wa kamba wanaume; nazo
timu za Ofisi ya Rais Ikulu, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Geita
Gold Mine (GGM) kila mmoja wamejikusanyia vikombe viwili, nazo timu za RAS
Iringa na Tumbaku ya Morogoro wote wamepata kikombe kimoja-kimoja.
No comments:
Post a Comment