GOLD COAST, Australia
WACHEZAJI nane wa timu
ya Cameroon inayoshiriki Michezo ya 21 ya Jumuya ya Madola inayoendelea hapa,
wametoweka katika makazi yao, viongozi wa timu wamesema.
Msemaji wa timu hiyo Simon
Molombe viongozi walibaini kutokuwepo kwa wachezaji hao na wameripoti tukio
hilo kwa polisi ya Australia.
Wachezaji hao watatu
ni wa kunyanyua vitu vizito na mabondia watano, ambao kwa mara ya mwisho
walionekana Jumatatu na Jumanne.
Cameroon imesema kuwa
kundi la wachezaji hao lilikuwa na viza halali ya Australia hadi Mei 15 mwaka
huu.
Viongozi wa timu hiyo
waliwataja wachezaji hao waliopotea kuwa ni wanyanyua vitu vizito Olivier Matam
Matam, Arcangeline Fouodji Sonkbou na Petit Minkoumba, wakati mabondia ni Christian
Ndzie Tsoye, Simplice Fotsala, Arsene Fokou, Ulrich Yombo na Christelle Ndiang.
"Mamlaka
imesikitishwa sana na kitendo cha wachezaji hao waliotoweka, wengine wakiwa
hata bado hawajaanza kushindana, “alisema Molombe.
"Tunatarajia
watarudi kijijini na kurudi nyumbani na wenzao.”
Serikali ya Australia
imewaonya wachezaji dhidi ya kukaa ndhini humo baada ya kumalizika kwa viza
zao.
Shirikisho la Jumuiya
ya Madola limesema kuwa watafuatilia hali hiyo lakini walisema kuwa wachezaji
wana “haki ya kusafiri huru” kwa kuwa wana viza zao.
Mwaka 2012, wachezaji
saba wa Cameroon walitoweka wakati wakiwa jijini London walipokwenda na timu
yao kushiriki Michezo ya Olimpiki.
No comments:
Post a Comment