Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuelekea msimu wa kombe la Dunia 2018, Kampuni
ya MultiChoice Tanzania kupitia king’amuzi chake cha DStv imezindua kampeni
mpya ifahamikayo kama DStv ni Moto!
DStv Moto itamuwezesha mteja kujiunga na huduma
iitwayo “DStv Now” na kutazama vipindi vya DStv wakati wowote mahali
popote ikiwa ni pamoja na kupata fursa
ya kuunganisha vifaa vitano (5) zaidi ikiwemo simu ya kiganjani, Tablet, Laptop
au Desktop pamoja na Runinga.
Hii
inamaanisha watu wa tano (5) tofauti wanaweza kutazama huduma ya DStv kupitia
vifaa vitano (5) tofauti kwa wakati mmoja na kwa akaunti moja tu ya malipo ya
mwezi!
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini
Dar es Salaa leo, Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Alpha Mria alisema
“Wakati tunaelekea kwenye mashindano
makubwa kabisa ya soka Duniani , yaani Kombe la Dunia la FIFA , tunampa
fursa mteja kutazama huduma ya DStv kwenye vifaa hadi vitano kwa wakati mmoja.
Hii itawaondolea wateja wetu usumbufu na sintofahamu hususani pale watu wengi wanapotaka
kutazama vitu tofauti wakati wowote mahala popote kwa wakati mmoja.“
Aliongezea kusema “Tumekuwa tukiboresha huduma zetu
kila uchao hususan kuongeza maudhui na pia kuwarahisishia wateja wetu utazamaji
wa vipindi mbalimbali tena kwa kiwango cha hali ya juu kabisa“ alisema Alpha na
kuongeza kuwa App hiyo ya DStv Now inapatikana kwa wateja wa vifurushi vyote.
Alpha amesema kwa kuzingatia uzito wa michuano ya
Kombe la dunia mwaka huu, DStv imejipanga kuhakikisha kuwa watanzania wanapata
fursa ya kuona mechi zote zikiwa katika mfumo wa HD, na pia kwa bei nafuu sana
na kwa jinsi watakavyo wateja.
“Kwanza tunakupa fursa ya kutazama kombe la
Dunia popote ulipo iwe ni kwenye laptop, tablet, simu, au kwenye runinga yako;
ni chaguo lako na ndiyo sababu tunasema Burudika popote ulipo na DStv.. DStv ni
moto!“
Pia amebainisha kuwa DStv itakuwa ikirusha matangazo
ya michuano hiyo kwa lugha ya kiswahili kwa kuwatumia watangazaji nguli wa
michezo hapa nchini. Amesema kuwa kumekuwa na maombi mengi sana kutoka kwa wateja
kutaka matangazo hayo yarushwe kwa kiswahili hivyo DStv imetimiza matakwa ya
wateja wake na sasa itarusha matangazo hayo kwa Kiswahili.
Kujiunga na huduma ya “DStv Now”, mteja anapaswa kupakua App ya DStv Now
kupitia Simu yake ya mkononi au Tablet ama Laptop na Desktop ataingia DStv.com
kisha kufuata maelekezo na kisha kujisajili kwa kuweka taarifa zake muhimu
ikiwemo email (barua pepe) namba ya simu pamoja na Smartcard number ya DStv.
Baada ya hapo mteja anaweza kufurahia huduma ya
DStv wakati wowote mahali popote. Huduma
hii inapatikana kwenye vifurushi vyetu vyote vya DStv.
Amewataka wateja wa DStv na watanzania kwa ujumla
kukaa mkao wa kula kwani kuna mambo makubwa sana kutoka DStv msimu huu wa kombe
la Dunia. “Huu ni mwanzo tu wa moto wa Kombe la Dunia, siku chache zijazo
tutasikia makubwa zaidi kutoka DStv kuhusu mashindano haya “
Kama hiyo haitoshi, kuanzia April 18 mwaka huu, DStv
iliongeza chanel maalum DStv 214 inayopatikana kwenye vifurushi vyote, ambayo ni mahususi kwa amsha-amsha za kombe
la Dunia.
Channel hii huelezea historia na matukio muhimu ya Michuano hiyo na
pia kuonyesha mechi kadhaa za michuano iliyopita bila kusahau makala maalum,
mahojiano na wadau na wataalamu mbalimbali wa soka na matukio yote yaliyotikisa
michuano hiyo kwa miaka iliyopita.
No comments:
Post a Comment