Na Mwandishi Wetu
MAANDALIZI ya
mbio za tatu za Heart Marathon zitakazofanyika Jumapili Aprili 29 jijini Dar es
Salaam, yamekamilika na kinachosubiriwa ni siku yenyewe ili kumpata mshindi.
Mratibu wa
Kamati ya Maandalizi ya Heart Marathon 2018, Peter Sabuni alisema leo kuwa,
kila kitu kimekwenda vizuri kwa upande wa maandalizi ikiwemo medali kwa
washiriki na watakaomaliza mbio za kilometa 21, 10, tano na meta 700 kwa
watoto.
Sabuni
alisema mbali na medali pia kamati imeshaandaa fedha taslimu kwa washindi,
ambazo kwa ujumla ni kiasi cha Sh milioni 16, ambapo washindi wa kwanza kwa wanaume
na wanake katika kiometa 21, kila mmoja ataondoka na kitita cha Sh milioni 2.
Mratibu wa Kamati ya Maandalizi ya Heart Marathon, Peter Sabuni akionesha medali watakaogawiwa washindi wa mbio hizo. |
Alisema kuwa
kingine, washiriki wote watapimwa afya zao, watapimwa uzito na urefu, shinikizo
la damu, kisukari, wingi wa mafuta mwilini na kupata ushauri wa kitaalam kutoka
kwa madaktari.
Alisema kuwa
nafasi za kujisajili kwa ajili ya kushiriki mbio hizo bado zipo, ambapo wakubwa
wanalipa Sh 30,000 wakati watoto ni Sh 20,000.
Wadhamini wa
mbio hizo ni pamoja na Tindwa Medical and Health Service, CBA, Nexlaw
Advocates, TCRA, TPB Bank, Sanlam Life Assurance, AGPAHI, AAR, Power Limited,
Jamii Forum, Samaki-Samaki, Issa Michuzi Blog, Azania Post.
Kwa mujibu wa
waandaaji, wanariadha kibao kutoka ndani na nje ya nchi tayari
wameshajiandikisha kwa ajili yam bio hizo, ambazo zitaanzia karibu na ufukwe wa
Coco, Oysterbayi na kupita katika mitaa mbalimbali kabla ya kumalizikia hapo
zilipoanzia.
No comments:
Post a Comment