Mchezaji
Sharifa Hamis (kulia) akifanya mazoezi ya kucheza bao na Ambakisye
Mwasunga (kushoto) wakifanya mazoezi ya kujiandaa na michuano ya Mei Mosi kwa
upande wa michezo ya jadi inayofanyika kwenye uwanja wa Somora mkoani Iringa.
Katikati ni mchezaji wa mchezo wa draft Bw. Omar Said akiangalia. (Picha na
Bahati Mollel-TAA)
TIMU
ya Ofisi ya Rais Ikulu imewachapa bila huruma wenyeji RAS Iringa kwa kuwafunga
magoli 49-8 katika mchezo wa netiboli wa michuano ya Kombe la Mei Mosi
uliofanyika kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCO) mkoani Iringa.
Ikulu
inayofundishwa na kocha mzoefu Mary Protas ambapo wafungaji wake Fatuma
Machenga aliibeba timu yake kwa kufunga magoli 48 huku Irene Elias alifunga bao
moja pekee. Magoli ya RAS Iringa yamefungwa na Warda Sapal na Zitaamanzia
Kididi kila mmoja manne.
Katika
mchezo wa soka timu ya RAS Iringa ilifungwa na Tumbaku ya Morogoro kwa magoli
3-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja w Samora.
Mshambuliaji Ramadhani Shegodo wa timu ya
Tumbaku ya Morogoro, akipiga mpira ulioandikia bao la kwanza dhidi ya RAS
Iringa, katika mchezo wa Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Samora.
Tumbaku wameshinda mabao 3-0.
Washindi
walipata bao lao la kwanza kupitia kwa Ramadhani Shegodo aliyefunga dakika ya
tisa baada ya kupata pasi kutoka kwa Mohamed Mtawal; huku bao la pili
lilipatikana dakika ya 29 kwa shuti kali
la Ushindi Nzogela.
Bao
la tatu lilifungwa na Salum Idd katika dakika 52 baada ya kupiga krosi murua
iliyomshinda kipa Mashaka Peter aliyejikuta akiusindikiza mpira langoni mwake.
Hatahivyo,
Tumbaku itabidi wajilaumu kwa kukosa magoli mengi ya wazi, ikiwemo dakika ya 20
mshambuliaji wake Issa Simbaliana kukosa penalti iliyotolewa na mwamuzi Steven Makuka baada ya
Nzogele kuchezewa rafu na Dickson Kiboye wa RAS Iringa, lakini kwa kupaisha
mpira juu ya goli,
Mfungaji Fatuma Machenga (GS) wa Ikulu
akifunga mbele ya mlinzi wa RAS Iringa (GK), Maria Mwita katika mchezo wa
netiboli wa mashindano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa
Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCO) Iringa. Ikulu wameshinda magoli 49-8.
Timu
za mchezo wa netiboli zitacheza kwa mtindo wa ligi kutokana na kuwa tano,
ambazo ni Uchukuzi, Ikulu, Hifadhi ya Ngorongoro, Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) na RAS Iringa, ambapo bingwa atapatikana kwa wingi wa pointi na
magoli ya kufunga.
Kwa
upande wa soka timu zimegawanywa katika makundi mawili, ambapo kundi ‘A’ linaundwa
RAS Iringa, Tumbaku, Tanesco na Hifadhi ya Ngorongoro, huku kundi ‘B’ zipo
Geita Gold Mine (GGM), Uchukuzi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Ofisi ya
Taifa ya Ukaguzi (NAO).
No comments:
Post a Comment