Na
Bahati Mollel-TAA, Iringa
TIMU
inayoundwa na wachezaji chipukizi ya Tumbaku ya Morogoro leo iliwavua ubingwa
wa michuano ya Kombe la Mei Mosi timu ya Geita Gold Mine (GGM) na kutinga hatua
ya fainali baada ya kuwafunga magoli 4-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu
fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Tumbaku
ambayo haijapoteza mchezo tangu ilipoanza hatua ya makundi ikiwa kundi ‘A’ na
GGM ikiwa kundi ‘B’ ilianza kupata bao lake la kwanza kupitia kwa mshambuliaji
wake Kelvin Makamba aliyepiga shuti kali nje ya 18 katika dakika ya pili.
GGM
walisawazisha katika dakika ya 44 kwa kichwa kilichopigwa na Oswald Binamungu baada
ya kupata pasi ya Ferdinand Makaranga.
Tumbaku
waliongeza bao la pili katika dakika ya 51 kupitia kwa mshambuliaji wake Issa Simbaliane
aliyepiga mpira wa faulu uliokwenda moja kwa moja golini, huku bao la tatu
lilipachikwa kimiani katika dakika ya 62 baada ya Emmanuel Mwakibinga
kuunganisha kwa kichwa kona iliyochongwa na Idd Likasi.
Kiungo
Idrisa Magongo alifunga kitabu cha magoli katika dakika ya 79 kwa kufunga bao
la nne.
Hatahivyo,
Katibu mkuu wa timu ya GGM, Wilhemin Bayanga pamoja na kukiri mchezo ulikuwa
mkali na mzuri lakini wameikatia rufaa timu nzima ya Tumbaku kwa madai
wamechezesha mamluki.
Katika
mchezo mwingine wa nusu fainali timu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)
imeingia fainali baada ya kuifunga timu ngumu ya Uchukuzi kwa magoli 2-1.
Uchukuzi ndio walikuwa wa kwanza kupachika bao katika dakika ya 67 kupitia kwa
Omary Kitambo.
Tanesco
walisawazisha kwa njia ya penalti iliyotolewa na mwamuzi Winfred Fyataga,
katika dakika ya 70 na Seleman Ismail baada ya kipa Willy Barton kumchezea
madhambi Gossage Mtumwa. Bao la ushindi
la Tanesco lilifungwa na Fortunatus Mgimba katika dakika ya 76 baada ya kipa
Barton kuusukumiza mpira wa kona uliochongwa na mfungaji.
Kocha
Mkuu wa Tanesco, Fidelis Almas amekiri leo atakuwa na kibarua kipevu kutokana
na Tambuku kutokana na wachezaji wake kuwa chipukizi zaidi.
“Ninajua
mechi itakuwa kali lakini tumejiandaa kukabiliana na Tumbaku kwani tunawajua
kutokana na kuwaona mara kadhaa wakiwa wanacheza na tulikuwa kundi moja,”
alisema Almas.
Wakati huo huo,
timu ya Uchukuzi imeongeza kikombe baada ya kushinda Mzee Omari Said kuibuka
bingwa katika mchezo wa bao uliofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa Iringa.
Ushindi wa pili ulichukuliwa na Suleiman Chitanda wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) na Shaaba Kidang’ala wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) aliibuka
wa tatu.
No comments:
Post a Comment