LONDON, England
VINARA wa Ligi Daraja la Kwanza Wolverhampton
Wanderers imepanda daraja na kufuzu kucheza Ligi Kuu ya England msimu ujao
baada ya mchezo wao wa juzi.
Timu hiyo imemaliza miaka sita ya kuwa nje ya Ligi
Kuu bila ya kucheza wakati wapinzani wao wa karibu Fulham kutoka sare ya
kufungana bao 1-1 dhidi ya Brentford, ambayo ilisawazisha katika dakika ya 94.
Wolves,ambao wana pointi 92 baada ya kucheza mechi 42,
ilikuwa ikihitaji pointi zingine nne kutoka katika mechi zao nne za mwisho ili
kushinda taji lakini wamepanda daraja kimahesabu.
Vinara hao wamejihakikishia nafasi hiyo ya kukipiga
Ligi Kuu bia utata wowote kufuatia kuwa karibu na wakala wa Kireno Jorge
Mendes.
Mendes ni wakala wa kocha mkuu Nuno Espirito Santo na
wachezaji nyota Ruben Neves, Diogo Jota na Ivan Cavaleiro. Pia ana uhusiano wa
muda mrefu na mmiliki wa klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment