Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangala. |
Na Mwandishi Wetu, Karatu
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangala leo
atabariki mbio za 11 za Ngorongoro Race zitakazofanyika mjini hapa na
kushirikisha wanariaha zaidi ya 700 kutoka ndani na nje ya nchi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa mbi hizo ambazo kauli
mbiu yake ni `Kimbiza Jangili’ Meta Petro, usajili wa wanaotaka kushiriki kwa
mbio hizo za kilometa 21, ulitarajia kukamilika leo tayari kwa mpambano
utakaofanyika kesho.
Alisema Kigwangala amethibitisha kuanzisha mbio hizo
na kukabidhi zawadi kwa washindi pale zitakapokamilika na washindi kujulikana.
Alisema mbio hizo zitaanzia katika lango kuu la kuingilia
na kutokea katika Bonde la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), ambao ndio
pia ni wadhamini wakuu wake na kumalizikia katika viwanja vya Mazingira Bora
katikati ya Mji wa Karatu.
Alisema kuwa wanatarajia mbio za mwaka huu zitakuwa
na ushindani wa hali ya juu, hasa ukizingatia zitashirikisha wanariadha wengi
zaid ya 500 walioshiriki mwaka jana.
Nyota mbalimbali wa mbio nchini wanatarajia kushiriki
mbio hizo wakiwemo washindi wa mwaka jana kwa upande wa kiume na kike, Faraja
Lazaro wa JKT na Failuna Abdi wa Talent Club ya Arusha, ambao walishinda mbio
hizo kwa kutumia saa 1:03.42 na 1:03.52.
Mshindi wa kwanza wa mbio hizo kwa upande wanaume na
wanawake, kila mmoja ataondoka na Sh milioni 1 wakati mshindi wa pili atabeba
Sh 500,00 huku watatu Sh 250,000, mshindi wan ne atapewa 100,000 na watano Sh
80,000.
Kwa mujibu wa waandaaji, mbio za mwaka huu zitakuwa
na zawadi hadi kwa mshindi wa 15 huku mshiriki yeyote atakayemaliza mbio hizo
katika nafasi yoyote, atapewa medali pamoja na fulana kama kumbukumbu za
kushiriki mbio hizo.
Mbali na kilometa 21 pia kutakuwa na mbio za kilometa
tano, ambapo kwa mara ya kwanza washindi watapewa zawadi, kwani mbio hizo ni za
kujifurahisha na waandaaji wamekuwa hawatoi zawadi kwa washindi.
Mshindi wa kwanza wa kilometa tano ataondoka na
kitita cha Sh 200,000 wakati mshindi wa
pili ataondoka na Sh 100,000 huku mshindi watatu kwa kila upande, atasepa na Sh
50,000.
Pia, kutakuwa na mbio za watoto wadogo, ambao
watachuana katika umbali wa kilometa 2.5, ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na
Sh 50,000, huku wa pili atabeba Sh 40,000 na watatu Sh 30,000.
Mbali na NCAA, wadhamini wengine ni Kampuni ya
Vinywaji Baridi ya Bonite Botlers.
No comments:
Post a Comment