Monday 31 December 2018

Michuano ya Emirates FA Cup Sasa Ndani ya DStv


Na Mwandishi Wetu
Wateja wa DStv wanauanza mwaka kwa kicheko baada ya kutangazwa rasmi kuwa DStv itaonyesha michuano maarufu ya ya Emirates FA Cup kupitia chaneli za SuperSport kuanzia tarehe 4 Januari 2019. Hii inamaana kuwa mechi za mzunguko wa tatu sasa zitaonekana katika kisimbuzi cha DStv.

Akizungumzia kurejea kwa michuano hiyo katika chaneli za SuperSport, Mkurugenzi wa MutiChoice Tanzania, Jacqueline Woiso amesema “Lengo letu ni kuwa mstari wa mbele katika kutoa burudani ya soka bora duniani kwa wateja wetu wa DStv hivyo, kuanzia tarehe 4 Januari 2019, wateja wetu wataweza kufurahia michuano ya Kombe la Emirates maarufu kama FA Cup kupitia chaneli za SuperSport zizopatikana ndani ya vifurushi vya DStv".

 Amesema kuwa muda wote MultiChoice imahakikisha kuwa wateja wake wanapata burudani ya hali ya juu na ndiyo sababu wamekuwa wakiongeza maudhui mapya kila uchao katika vifurushi vya DStv.

Sambamba na mechi za michuano ya kombe la FA za mzunguko wa tatu zitakazoanza Januari 4 2019, wateja wa DStv pia wataendelea kuburudika na ligi kubwa za soka zinazotamba duniani ikiwemo ligi kuu ya Uingereza maarafu kama PL, ligi kuu ya Italia Seria A, michuano ya ligi kuu ya Hispania {La Liga} na ligi ya mabingwa Ulaya maarufu kama EUFA Champions League bila kusahau maudhui  mengineyo mengi zikiwamo filamu na tamthilia mpya kutoka nje na ndani ya Tanzania na vipindi vya watoto.

Mechi hizi za michuano  ya Kombe la FA zitakuwa zikipatikana mubashara kupitia chaneli za Supersport ndani ya DStv. Idadi ya mechi zitakazoonekana mubashara zinatofautiana kulingana na aina ya kifurushi huku baadhi ya mechi hizo zikionekana katika kifurushi cha chini cha DStv Bomba kwa Sh 19,000.

Kwa wateja wanaotaka kujiunga na DStv, bado wanaweza kunufaika na ofa inayoendelea ya msimu wa sikukuu ambapo kwa gharama ya Sh.79,000 tu!  Mteja anapata seti kamili ya DStv. Pia kupitia mtandao wa bongoshop.dstv.com mteja anaweza kupata maelekezo ya ziada ya namna ya kujiunga na DStv, ikiwemo kuunganishwa na mawakala na mafundi wa DStv popote alipo.


Tuesday 18 December 2018

Ndege Mpya Mbili za ATCL Kuwasili Jumapili


Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Richard Mayongela akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele.

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema ndege mpya mbili za ATCL zinatarajiwa kutua Jumapili zikitokea nchini Canada tayari kwa kuanza kufanya kazi ya kusafirisha abiria.

Aidha, aliwaondoa watu hofu kuwa kusimamishwa kwa huduma za ndege ya Fastjet hakutawaathiri kwa vile wamejipanga kusafirisha abiria usiku na mchana ili kuhakikisha hawapati shida ya usafiri.

Akizungumza na waandishi wa habari,  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele alisema ndege hizo zitatua kama ratiba haitabadilika, kwani wameshapeleka rubani na wahudumu wa ndege kwenda nchini humo kwa ajili ya kurudi nazo.

“Mtengenezaji alituahidi mpaka Desemba 23, mwaka huu zitakuwa ziko tayari kurudi kuja kuanza kazi,  tayari tumepeleka wahudumu wa kuja nazo,”alisema.

Waziri huyo aliwatoa hofu Watanzania kuwa  hakuna atakayepata shida ya usfiri wa ndege kwani wamejipanga kwa viwanja vyenye taa kusafiri mpaka usiku na vile visivyokuwa na taa kama Songwe wataongeza ndege kutokana na uhitahiji ili watu wasikose usafiri kwenda na kutoka maeneo yote.

Aliwataka wahudumu wote wa ndege  na wale wa Mamlaka ya Usafiri wa  nchi Kavu na Majini (Sumatra) waliokwenda likizo kurudi haraka kusimamia huduma hizo hasa kipindi hiki cha sikukuu na kuhakikisha nauli haziongezwi upande wa mabasi yaendayo mikoani.

Alizungumzia kuhusu Fastjet kupewa notsi ya siku 28 kwa ndege hiyo kusitisha huduma baada ya kushindwa kulipa madeni yake na kutokidhi huduma za abiria na kwamba hawataruhusiwa kuruka popote hadi kuyalipa ikiwemo huduma, mishahara wanazodaiwa.

Pia Waziri Kamwele aliwataka viongozi na wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuhakikisha wanafanyia kazi malalamiko ya abiria wanayoyatoa juu ya mapungufu katika viwanja vya ndege vikiwemo vipoza hewa katika eneo la pili la kuwasili na kuondokea abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Juliuys Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Alisema abiria wamekuwa wakilalamika kuhusu joto lililopo Terminal Two, lakini wahusika hawajachukua hatua yoyote ya kurekebisha na wameendelea kufanya kazi kimazoa tu wakati hiki ni kipindi cha ushindani.

Pia alisema mtandao nao haufanyika  kazi vizuri, hivyo aliwataka TAA kuchukua hatua haraka kurekebisha matatizo hayo, sivyo kuanzia mwakani atachukua hatua kali.

Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Richard Mayongela aliomba muda ili kufanyia kazi mapungufu hayo na kusema atachukua hatua za kiutawala kuhakikisha mambo yanakuwa sawa haraka iwezekanavyo.

Mayongela pia aliwataka waandishi wa habari kuwa makini kwa kuandika au kutangaza habari kutoka katika vyanzo vya uhakika au rasmi na sio kupokea taarifa upande mmoja tu, tena kutoka katika mitandao.

Waziri alitoa muda hadi Januari mwakani kufanyia kazi changamoto hizo na ikiwa watashindwa basi wajiondoe wenyewe huku akisisitiza kuwa, sehemu ya tatu ya abiria ya Kiwanja cha Ndeger cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), kinatarajia kuanza kutumika Mei mwakani.

Friday 14 December 2018

Wanariadha Arusha Watamba Riadha ya Wazi


Viongozi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) kabla ya kuanza kwa mbio za kilometa 10 za mashindano ya wazi ya taifa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha leo.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
MASHINDANO ya wazi ya taifa ya riadha ya Ngorongoro ‘Ngorongoro National Open Athletics Championships’ yamefanyika leo jijini Arusha na kushuhudiwa na watazamaji kibao waliofika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid huku wanariadha wa Arusha wakitamba.

Tofauti na mashindano hayo yanapofanyikia jijini Dar es Salaam, leo uwanja huo ulikuwa na watazamaji kibao walioshuhudia wanariadha  wao, wengi wakitokea Arusha wakitamba katika mbio na michezo mbalimbali.
 
Mashindano hayo yalidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa mara ya kwanza katika mashindano ya taifa yalishirikisha mbio za barabarani za kilometa 10 badala ya zile za uwanjani za meta 10,000, ambazo  jana hazikuwepo.
 
Katika mbio za kilometa 10, Jackson Mwakombe alimaliza wa kwanza kwa kutumia dakika 32:00.22, baada ya kuongoza kwa muda mrefu mbio hizo akiwaacha wenzake mbali.
Wanariadha wakichuana katika mbio za meta 5,000 za mashindano ya wazi ya taifa jijini Arusha leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
 Arusha pia ilitwaa medali ya dhahabu katika kilometa 10 kwa wanawake wakati Neema Kisuda alipomaliza wa kwanza kwa kutumia dakika 40:01.04 akifuatiwa na wanariadha wengine wa Arusha, ambao ni Gloria Makula na Sarah Hiti waliomaliza katika nafasi ya pili na tatu kwa dakika 40:27.98 na 41:26.91.

Benjamin Michael alimaliza wa kwanza kwa kutumia sekunde 10:99, huku Laurent Masatu na Bakari Barnabasi wote wa Arusha wakimaliza katika nafsi ya pili na tatu kwa kutumia sekunde 11:10 na 11:18.
Mwanariadha kipita mbele ya bango la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ambao ni wadhamini wa mbio za wazi za taifa zilizofanyika leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Katika mbio za meta 800, Mariam Salim, Grace Jackson na Shamin Ramadhani wote wa Arusha walimaliza kwa dakika 2:18.09, 2:20.72 na 2:21.87 na kushika nafasi ya kwanza, ya pili na tatu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Kwa upande wa meta 5,000 wanawake, Arusha ilishika nafasi mbili za kwanza pale, Natalia Elisante na Angelina Daniel walimaliza wa kwanza kwa kutumia dakika 16:54.52 na 17:18.80 huku Angelina John wa Singida akimaliza wa tatu kwa kutumia dakika 18:10.68.
Ni hatari lakini salama! Mwanariadha Jackson Makombe akipita eneo la Njiro huku magari nayo yakipita wakati wa mbio za kilometa 10 za mashindano ya wazi ya taifa jijini Arusha leo. Makombe alishinda mbio hizo kwa dakika 32:00.22.
Katika mbio za meta 800 kwa wanaume, mwanariadha wa Manyara Gabriel Geay alitamba baada ya kumaliza wa kwanza kwa kutumia dakika 1:50.75 huku akifuatiwa na Faraja Damas na Simon Francis wote wa Arusha waliotumia muda wa dakika 1:52.28 na 1:52.68.

Washindi wa kwanza katika kila mchezo wa mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, waliondoka na Sh 150,000 kila mmoja wakati wale walioshika nafasi za pili kila mmoja alipata 100,000 na watatu Sh 50,000.
Watoto nao walichuana katika mbio za meta 100 wakati wa mashindano hayo ya wazi ya taifa leo Sheikh Amri Abeid.
 Washindi wa kwanza wa michezo yote kuanzia ile ya kilometa 10, meta 5,000,  meta 100, meta 800, kuruka chini, meta 400, meta 1500, meta 200 na wale wa kupokezana vijiti, wote kesho watatembelea hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, ikiwa ni ofa kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo.
Wanariadha wakike wakichuana katika mbio za meta 5,000.

Mwanariadha akiruka chini wakati wa mashindano ya wazi ya taifa ya riadha leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Tuesday 11 December 2018

TAA Waendelea Kutoa Kwa Jamii,Yasaidia Tamasha la Ngoma


Mratibu wa Tamasha la Ngoma za Utamaduni na Maonesho ya Biashara la Chato, Amon Mkoga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo katika Kijiji cha Makumusho Jiini Dar es Salaam leo. Tamasha hilo la tatu litafanyika Chato mkoani Geita Desemba 22, 2018. Kulia ni Meneja  Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). 

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kufanikisha shughuli mbali mbali za jamii, kwa kutoa misaada yenye tija.


Hilo limekuwa bayana leo tarehe 12 Disemba, 2018 kwenye Kijiji cha Makumbosho Jijini Dar es Salaam, ambapo TAA imetoa msaada wa fulana 100 kwa ajili ya kufanikisha Tamasha la Utamaduni la Chato linalotarajiwa kufanyika tarehe 22 Disemba, 2018 katika Uwanja wa Mazaina Chato.

Akizungumza katika Mkutano wa waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TAA, Bw. Abdi Mkwizu amesema Mamlaka ina wajibu mkubwa wa kuunga mkono shughuli za kijamii, kwa kutoa misaada ya mbalimbali.

   Kaimu Mkurugenzi wa Rasimali Watu na Utawala wa Viwanja vya NdegeTanzania (TAA), Abdi Mkwizu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la za Utamaduni la Chato katika Kijiji cha Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam leo. 
“Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania ina wajibu wa Kusimamia, kuendesha, kuboresha na kuendeleza Viwanja vya Ndege Tanzania lakini pia mbali na kutoa huduma hizo tuna wajibu wa kushiriki katika shughuli za kijamii, kwa wadau ambao wanatufanya sisi tuwepo,” amesema Bw. Mkwizu.

Pia Bw. Mkwizu amebainisha kwamba TAA inahudumia Viwanja 58 vilivyopo Tanzania Bara chini ya serikali, hivyo ni wajibu wao kushiriki katika shughuli za kusaidia jamii sehemu yeyote ile kulingana na uhitaji na bajeti iliyopo.



 Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Bw. Habbi Gunze (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Tatu la  za Utamaduni katika Kijiji cha Makumbusho. Kulia ni Meneja Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),Abdi Mkwizu na mwingine ni mratibu wa tamasha hilo, Amon Mkoga. Tamasha hilo litafanyika Chato mkoani Geita.


“Ikumbukwe siku za hivi karibuni TAA tumeshirika katika kufanikisha Tamasha la Urithi Wetu lililofanyika kuanzia Oktoba Mosi mpaka Oktoba 7, 2018 katika Kijiji cha Makumbusho, tumetoa pia msaada wa Mafuta Kinga jua ya Ngozi kwa watoto wenye ulemavu wa Ngozi katika baadhi ya shule hapa Dar es Salaam, lakini pia tarehe 24 Novemba mwaka huu tumekabidhi Shule ya Msingi ya Kisasa huko Bukoba inaitwa Tumaini,  na tunaamini itaongeza ufaulu kwa wanafunzi huko Bukoba na hayo ni macheche kati ya mengi ambayo Mamlaka inafanya kwa Jamii” amebainisha Bw. Mkwizu.
Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Abdi Mkwizu (kulia) akikabidhi moja ya fulana,zilizotolewa na TAA kwa ajili ya Tamasha la Ngoma za Utamaduni la Chato, linalotarajia kufanyika Desemba 22, 2018.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu na niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Bw. Habbi Gunze ameishukuru Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa mchango wake kufanikisha Tamasha la Utamaduni la Chato.

“Niwashukuru sana Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa mchango wao nap engine bila wao hili la leo lisingeweza kufanikiwa. Utamaduni ndio uhai wa Taifa, kwa hiyo nchi isipokua na Utamaduni nchi inakua sio hai, hivyo kwa Mchango huu wa kusaidia hili nawapongeza sana TAA” amesema Bw. Gunze.
Mcheza ngoma za asili, Bw,. Ally Mango akicheza na nyoka mbele ya waandishi wa Habari katika kikiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, wakati wa utoaji wa fulana 100 kwa tamasha la Utamaduni la Chato zilizotolewa leo na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).  (PICHA ZOTE KWA HISANI YA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA)
Naye Mkurugenzi wa Chief Promotions ambaye ndie mratibu wa Tamasha hilo Bw. Amon Mkoga amesema kwamba Tamasha litakuwa na mambo yote ya kiutamaduni ili kuenzi asili ya Kitanzania.

“Kauli mbiu ya Tamasha la Utamaduni la Chato inasema “Maendeleo ya Viwanda yasiache Utamaduni nyuma” ambapo Tamasha hili ni maalum kwa ajili ya kuuenzi utamaduni wa Mtanzania. Katika Tamasha hili kutakua na Vikundi mbalimbali vya Utamanduni. Vikundi vya ngoma vitakuwepo kutoka Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Tabora na Chato wenyewe, hivyo tunawaomba wananchi mtusaidie kufikisha taarifa hizi kwa watanzania” ameeleza Bw. Mkoga.
Mkurugenzi wa Chief Promotions Bw. Amoni Mkoga (katikati), Mwenyekiti Bodi ya Baraza la Salaa la Taifa (BASATA), Bw. Habbi Gunze (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Abdi Mkwizu, wakionesha vipeperushi vya Tamasha la Ngoma za Utamaduni la Chato.
Tamasha la Utamaduni la Chato ni tamasha kubwa la ngoma ambalo hufanyika kila mwaka na hii itakua ni mara ya tatu mfululizo likifanyika Chato mkoani Geita.





Saturday 1 December 2018

Mahafali Pre-Unit Shule za Filbert Bayi Yafana

Wahitimu wa darasa la Pre-Unit wa Shule za Filbert Bayi wakipozi kwa picha kabla ya kupiga picha ya pamoja na mgeni rasmi Naibu waziri wa Nishati na Madini, Subira Mgalu Mkuza, Kibaha leo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Subira Mgalu (kushoto) akiwasili katika shule za Filbert Bayi Mkuza leo. Kulia ni Mkurugenzi wa shule hizo, Anna Bayi.


Wanafunzi wa Pre-Unit wa shule za Filbert Bayi wakiwa na mgeni rasmi kabla ya mahafali yao leo Mkuza, Kibaha mkoani Pwani.


Wazazi wa wahitimu wa Pre-Unit wa Shule za Filbert Bayi pamoja na wageni waalikwa wakati wa mahafali leo Mkuza, Kibaha mkoani Pwani.

Wazazi na waalikwa wakati wa mahafali ya Pre Unit leo.

Wahitimu wa Pre Unit wakiongozwa na mwalimu wao wakati wa kuingia katika ukumbi leo.

Pre Unit wakicheza wakati wa mahafali yao leo Mkuza, Kibaha.



Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Subira Mgalu (wa pili kulia) akiwatuza wanafunzi wa Pre Unit baada ya kukunwa na uchezaji wao wakati wa mahafali yao leo. Kulia ni Mkurugenzi wa shule hizo, Anna Bayi.


Tuesday 27 November 2018

Waziri Kamwelwe Aitaka TBA kuwa na Subira



1.        Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe  (mwenye suti ya bluu) akiwaeleza jambo wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Ihungo ya Kagera, alipofanya ziara hivi karibuni. Kulia (mwenye suti ya udongo ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Bw. Philip Boniventura.


·Aridhishwa na Ujenzi wa Ihungo Boys

Na Mwandishi Wetu, Bukoba
WAKATI Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe ameomba taasisi za serikali, Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wizara, ambazo zimeipa kazi Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA), kuwa na subira kwa kuwa inaupungufu wa wafanyakazi, lakini ameridhishwa na ujenzi wa shule ya sekondari ya Wavulana ya Ihungo ya mkoani Kagera iliyojengwa na taasisi hiyo.

Akifafanua Mhe. Kamwelwe amesema TBA wanakumbwa na changamoto kubwa ya upungufu wa wafanyakazi, ambapo kwa Tanzania nzima wanawafanyakazi 300 pekee, ambao wanajitoa kwa kufanya kazi kwa bidii, ambapo idadi kamili inayotakiwa ni wafanyakazi 1,700.


1.        Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA) mkoa wa Kagera, Mhandisi Herico Bahati (mwenye shati la batiki) akimpa maelezo mbalimbali Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kushoto) kuhusiana na ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Ihungo, waliyoijenga baada ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2016. Mbele ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Philip Boniventura.


Hatahivyo, ameipongeza TBA kwa kufanya kazi nzuri za ujenzi wa majengo mbalimbali ya serikali kwa kutumia thamani halisi ya fedha, tofauti na wakandarasi binafsi, ambao  wamekuwa na gharama kubwa.

“Utendaji wa TBA bado unaleta mashaka nchi nzima na nimefanya nao kikao nikabaini wapo wafanyakazi 300 pekee na wanatakiwa angalau 1000 ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, hivyo nashauri pamoja na kusikia malalamiko kila upande kutoka kwa Wakuu wa Wilaya, Mikoa, Bungeni na Watendaji wengine wa serikali, ninayafanyia kazi likiwemo la uhaba wa wafanyakazi,” amesema Mhe. Kamwelwe.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA) mkoa wa Kagera, Mhandisi Herico Bahati (mwenye shati la batiki) akimpa maelezo mbalimbali Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kushoto) kuhusiana na ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Ihungo, waliyoijenga baada ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2016. Mbele ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Philip Boniventura.
Baadhi ya kazi za ujenzi wanazofanya na walizofanya TBA ni pamoja na ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mkoani Dodoma; ujenzi wa hospital ya Mkoa wa Simiyu na Ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma mikoa mbalimbali.

Akizungumzia ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Katika hatua nyingine, Mhe. Kamwelwe ameipongeza TBA kwa ujenzi wa shule ya kisasa ya sekondari ya wanaume ya Ihungo iliyoathirika na tetemeko la ardhi lililotokea Kagera 2016.

“Nawapongeza sana kwa kujenga shule nzuri tena kwa gharama nafuu ya Bil. 10.4, ukiangalia wengine walitaka kujenga kwa Bil. 36, hivyo TBA wameokoa fedha nyingi sana za Watanzania na kiwango chao cha kazi ni kizuri,” amesema Mhe. Kamwelwe.


1.        Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Wavulana ya Ihungo na wa shule ya sekondari Bukoba, wakinawa mikono katika mabomba ya kisasa, ambayo yamejengwa na Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA) baada ya shule hiyo kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2016.

Naye Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Kagera, Mhandisi Herico Bahati amesema ujenzi wa shule hiyo ulianza Oktoba 5, 2016, ambapo kuna majengo matatu ya ghorofa ya madarasa yenye vyumba 24, ofisi 12 za walimu, jengo la vyoo 80, mabweni matatu yenye vyumba 96, nyumba 30 za walimu, upanuzi wa bwalo la chakula na wamechimba kisima cha maji.

Shule hiyo inawanafunzi 600, ambapo sasa pia imeongezewa wanafunzi 751 wa shule ya Sekondari ya Bukoba waliohamishiwa hapo kwa muda baada ya shule yao kuezuliwa paa na upepo mkali uliotokea Oktoba 2018.

Nyumba nne kati ya 30 za walimu wa shule ya sekondari ya wavulana ya Ihungo ambao zimejengwa sambamba na vyumba vya madarasa na mabweni na Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA), baada ya shule ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililoikumba Mkoa wa Kagera mwaka 2016.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba, ambaye pia anakaimu wilaya ya Bukoba Mjini, Mhandisi Richard Ruyangu ameishukuru serikali kwa kuijenga tena shule hiyo na sasa wanafunzi wanaendelea na masomo.

“Tunaishukuru serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa kutujengea tena shule nzuri na tunaimani kwa mazingira haya watoto watasoma kwa bidii, na hata walimu hali kadhalika watafundisha kwa moyo tumeona wamejengewa nyumba nzuri na za kisasa tena zipo maeneo ya karibu na shule itakuwa hawatoki mbali kuja kufundisha,” amesema Mhandisi Ruyangu.


1.        Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Ihungo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe wakati alipotembelea shule hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi wake. Shule hiyo imejengwa na Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA) baada ya kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2016.


Kiranja mkuu wa shule hiyo, Athuman Mohamed kwa niaba ya wanafunzi wenzake, ameishukuru serikali kwa kuwajengea tena shule yao na wameahidi kusoma kwa bidi ili kufanya vizuri katika masomo yao

.

Monday 26 November 2018

Matokeo Yoote Mashindano ya Riadha ya Taifa Wanawake 2018


2ND FIRST LADIES COMPETITION
NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM 24TH  – 25TH /11/2018

RESULTS
Wanariadha kutoka mikoa mbalimbali wakichuana katika mbio za Meta 10,000 za Mashindano ya Riadha ya Taifa ya Wanawake kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
100M HEAT 1
POS
NAME
REGION
TIME
1.
KAZIJA HASSAN SIMAI
MJINI MAGHARIBI
12.60
2.
KEFLEN KIPILI
MBEYA
13.44
3.
JOHARI HUSSEN
TABORA
13.56
4.
RUSIA NDEKI
GEITA
13.57
5.
JULIETH PHITA
MBEYA
13.80
6.
GRACE SINZA
SIMIYU
13.94
7.
REHEMA SELEMAN
MTWARA
14.00
8.
ANASTAZIA KAPINGU
RUVUMA
14.86
9.
SUBIRA MWANGATA
LINDI
15.93

100M HEAT II
POS
NAME
REGION
TIME
1.
WINFRIDA MAKENJI
DAR ES SALAAM
13.73
2.
NASRA ABDALLAH
KUSINI UNGUJA
13.88
3.
SUBEHA HAMAD
KUSINI PEMBA
14.16
4.
VICTORIA BABUYA
SONGWE
14.17
5.
MESIA GIDEON
MBEYA
14.19
6.
RABEKA KASHINDYE
NJIOMBE
14.35
7.
JANETH MICHAEL
TANGA
14.69
8.
GETRUDE DUE
RUVUMA
15.16

Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi (kulia) akizungumza na Katibu mkuu wa Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday na kocha wa riadha Mmarekani, Ron Davis (kushoto).
100M HEAT III
POS
NAME
REGION
TIME
1.
NURU NASIB MAKAME
KUSINI MAGHARIBI
13.74
2.
AGRIPINA INUS
MWANZA
13.94
3.
ZAWAD JUMA
MARA
14.03
4.
NYAMIZI MATHEO
TABORA
14.29
5.
NEIRA ERICK
LINDI
14.30
6.
ROZA BONIFACE
SONGWE
14.54
7.
ANNE PETER
MTWARA
15.20
8.
MWANAMWEMA KOMBA
PWANI
15.97

100M HEAT IV
POS
NAME
REGION
TIME
1.
SHUWENA ALLY
KASKAZINI UNGUJA
12.73
2.
JANE MAIGA
ARUSHA
12.89
3.
LEOCADIA JOHN
TABORA
13.90
4.
FIDEA JOSEPHAT
SINGIDA
13.92
5.
AGATHA MWINGA
DODOMA
13.95
6.
FATUMA ABDALLAH
KASKAZINI UNGUJA
13.95
7.
MARIA KATITI
SONGWE
14.31
8.
ANITHA BROWN
DAR ES SALAAM
14.67

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, William Kalaghe akisoma risala wakati wa ufungaji wa mashindano ya taifa ya riadha ya wanawake kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
100M   FINAL
POS
NAME
REGION
TIME
1.
KAZIJA HASSAN SIMAI
MJINI MAGHARIBI
12.20
2.
WINFRIDA MAKENJI
DAR ES SALAAM
12.21
3.
NASRA ABDALLAH
KUSINI UNGUJA
12.26
4.
HIMIDIYA OMARY
KUSINI UNGUJA
12.28
5.
SHUWENA ALLY
KASKAZINI UNGUJA
12.35
6.
JOHARI HUSEIN
TABORA
12.37
7.
KEFLENI KIPILI
MBEYA
12.53
8.
RUSIA NDEKI
GEITA
12.85
9.
JANE MAIGA
ARUSHA
13.16
10.
AGRIPINA INUS
MWANZA
13.79



200M HEAT I
POS
NAME
REGION
TIME
1.
NAIMA MUSSA
MJINI MAGHARIBI
26.56
2.
KEFLENI KAPILI
MBEYA
26.65
3.
ZAINABU ALLY
KASKAZINI
28.47
4.
ZAWADI JUMA
MARA
30.60
5.
ADELINA AHUNGU
MOROGORO
30.74
6.
EDIKEDNESS MWISIGWA
KILIMANJARO
30.74
7.
NEILA ERICK
LINDI

8.
AISHA ALLY
TANGA


200M HEAT II
POS
NAME
REGION
TIME
1.
JANE MAIGA
ARUSHA
27.42
2.
NASRA ADBALLAH
KUSINI MAGHARIBI
28.58
3.
MARTHA STANSLAUS
GEITA
28.97
4.
ANASTAZIA KAPINGA
RUVUMA
28.99
5.
HALIMA ATHUMAN
TENGA
29.66
6.
MARIA KATITI
SONGWE
30.94

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ndumbalo wakati wa ufungaji wa mashindano ya riadha ya wanawake jana.
200M HEAT III
POS
NAME
REGION
TIME
1.
WINFRIDA MAKENKII
DAR ES SALAAM
26.09
2.
SHUWENA A. MUHAMED
KASKAZIN UNGUJA
26.51
3.
THEREZA BENALD
SIMIYU
27.72
4.
AGRIPINA YUNUS
MWANZA
28.62
5.
JULIETH FITA
MBEYA
29.41
6.
ESHA SORO
LINDI
36.03

200M HEAT IV
POS
NAME
REGION
TIME
1.
HIMIDIA OMARY
KUSINI MAGHARIBI
26.87
2.
GRACE SINZA
SIMIYU
28.43
3.
VICTORIA BABUYA
SONGWE
29.50
4.
NYAMIZI MATHEO
TABORA
29.63
5.
MESIA GIDION
MBEYA
29.90
6.
ANASTINA LEONARD
KATAVI
31.59
7.
OLIVIA EMANUEL
KAGERA
41.74

200M HEAT V
POS
NAME
REGION
TIME
1.
SUBEHA HAMADI
KUSINI PEMBA
27.82
2.
DESIANA SINGAILE
IRINGA
28.09
3.
MARIAM MAKOYE
KILIMANJARO
29.00
4.
REHEMA SULEMAN
MTWARA
30.03
5.
ROZA BONIFACE
SONGWE
30.28
6.
BIHIJA ABIED
DODOMA
30.53

200M HEAT VI
POS
NAME
REGION
TIME
1.
KAZIJA HASSAN
MJINI MAGHARIBI
26.02
2.
MARY EMIL
DSM
27.63
3.
RUSIA NDEKI
GEITA
29.03
4.
AGNES KWABI
TABORA
30.47
5.
PILI MWIPI
IRINGA
38.00
6.
FATUMA MASHAKA
MOROGORO
38.47

200M  SEMI FINAL  HEAT 1
POS
NAME
REGION
TIME
1.
HIMIDIA OMARY
KUSINI UNGUJA
25.82
2.
NAIMA MUSSA
MJINI MAGHARIBI
26.30
3.
SUBEH HAMAD
KUSINI PEMBA
26.88
4.
KEFLIN KIPILI
MBEYA
27.38
5.
GRACE SINZA
SIMIYU
28.60
6.
DESIANA SINGAILE
IRINGA
28.62
7.
MARIA MAKOYE
KILIMANJARO
29.37
8.
ZAINAB ALLY
KASIKAZINI UNGUJA
29.55

200M  SEMI  FINAL  HEAT II
POS
NAME
REGION
TIME
1.
WINFRIDA MAKENJI
DSM
25.58
2.
NASRA ABDALLAH
KUSINI UNGUJA
25.84
3.
KASIJA HASSAN SIMAI
MJINI MAGHARIBI
25.91
4.
SHUWENA A. MOHAMED
KASIKAZINI UNGUJA
26.16
5.
JANE MAIGA
ARUSHA
26.28
6.
MERRY EMIL
DSM
27.23
7.
THEREZA BENALD
SIMIYU
28.05
8.
MARTHA STANSLAUS
GEITA
28.31

200M    FINAL 
POS
NAME
REGION
TIME
1.
KAZIJA HASSAN SIMAI
MJINI MAGHARIBI
25.53
2.
NASRA ABDALLAH
KUSINI UNGUJA
25.75
3.
WINFRIDA MAKENJI
DAR ES SALAAM
25.90
4.
SHUWENA ALLY
KASKAZINI UNGUJA
25.97
5.
JANE MAIGA
KUSINI UNGUJA
26.06
6.
JANE MAIGA
ARUSHA
26.20
7.
SARAYA OTHUMAN
MJINI MAGHARIBI
26.37
8.
SUBEYA HAMAD
KUSINI PEMBA
26.68

400M  HEAT  I
POS
NAME
REGION
TIME
1.
PILI MIPAWA
PWANI
59.71
2.
HIMIDIA OMARY
KUSINI UNGUJA
61.70
3.
MARY EMMILY
DAR ES SALAAM
62.81
4.
JOHARI HUSSEIN
TABORA
62.84
5.
THEREZA BENALD
SIMIYU
63.50
6.
NURU NASIBU
KUSINI PEMBA
65.50
7.
HALIMA ATHUMAN
TANGA
65.76

400M  HEAT  II
POS
NAME
REGION
TIME
1.
REGINA DEOGRATIUS
PWANI
58.59
2.
CLEMENGIDA MKULILEI
PWANI
60.37
3.
ZULEHA OMARY KOMBA
KUSINI UNGUJA
63.56
4.
MATHA STANSLAUS
GEITA
64.63
5.
ROSE SEIF
ARUSHA
64.80
6.
ZAINABU ALLY OTHMAN
KASKAZINI UNGUJA
66.61




400M  HEAT  III
POS
NAME
REGION
TIME
1.
MARIAM SALIM
ARUSHA
60.26
2.
SALAYA OTHMAN
MJINI MAGHARIBI
63.26
3.
MARIETHA NOELELA
MWANZA
64.84
4.
HADIJA HAJI MAKAM
MJINI MAGHARIBI
66.97
5.
ANASTINA LEONALD
KATAVI
75.16
6.
ENEA MLALILA
SONGWE
82.08

400M HEAT IV
POS
NAME
REGION
TIME
1.
RUSIA PIUS
MWANZA
62.58
2.
LEOCADIA JOHN
TABORA
65.75
3.
VICTORIA MATAI
KILIMANJARO
69.44
4.
GETRUDA DUWE
RUVUMA
71.84
5.
VIOLETH RENATUS
RUVUMA
77.52
6.
NEEMA ENDREW
KAGERA
82.62
7.
ANNE PETTER
MTWARA
90.18

400M FINAL
POS
NAME
REGION
TIME
1.
HIMIDIA OMARY
KUSINI UNGUJA
58.72
2.
REGINA DEOGRATIUS
PWANI
58.79
3.
MARIA SALUM
ARUSHA
59.56
4.
PILI MIPAWA
PWANI
60.38
5.
HELEMENGILIDA NGULICE
PWANI
62.85
6.
RUSIA PIUS
MWANZA
63.70
7.
SARAYA OTHMAN
MJINI MAGHARIBI
64.33
8.
LEOKADIA JOHN
TABORA
65.19

800M HEAT I
POS
NAME
REGION
TIME
1.
REGINA MPIGACHAI
PWANI
2:13.5
2.
FAIZA ALLY
SINGIDA
2:18.70
3.
ZAKIA SAIDA
SINGIDA
2:21.41
4.
ROZALIA FABIAN
ARUSHA
2:22.85
5.
AISHA MZUMARI
MARA
2:26.25
6.
FATUMA ALLY
KASKAZINI
2:33.99
7.
MARIETA NGELELA
MWANZA
2:35.03
8.
KEDNESS MWESIGWA
KILIMANJARO
2:43.25
9.
TAUSI SAID
RUVUMA
2:45.38
10.
NYANZOBE MAGINA
SIMIYU
2:46.05
11.
LOVENESS ENOSI
KATAVI
2:46.97
12.
HELLEN VALENTINO
KILIMANJARO
3:03.77

800M HEAT II
POS
NAME
REGION
TIME
1.
DORCAS BONIFACE
PWANI
2:18.15
2.
KISA ABDALLAH
MBEYA
2:19.57
3.
AISHA LUBUNA
ARUSHA
2:21.62
4.
ROSEMARY GUSTAPH
KUSINI UNGUJA
2:21.93
5.
CATHERINE AMRI
TABORA
2:25.75
6.
ZAYANA MBEDULE
IRINGA
2:30.18
7.
MARIAM LIGWA
GEITA
2:33.65
8.
LETICIA KIDILA
SIMIYU
2:35.58
9.
VICTORIA NATAY
KILIMANJARO
2:50.22
10.
ENEA MLALILA
SONGWE
3:18.96

800M FINAL
POS
NAME
REGION
TIME
1.
REGINA DEOGRATIUS
PWANI
2:11.07
2.
MARIAM SALIMU
ARUSHA
2:18.03
3.
DORCAS BONIFACE
PWANI
2:18.87
4.
AISHA RUGUNA
ARUSHA
2:20.59
5.
FAIZA ALLY
SINGIDA
2:20.85
6.
RUSIA PIUS
MWANZA
2:22.88
7.
KUZA ABDALAH
MBEYA
2:23.19
8.
YUSTA NINGA
MANYARA
2:23.62
9.
ROSEMARY GUSTUS
KUSINI UNGUJA
2:23.90
10.
ZAKIA SAID
SINGIDA
2:24.27





1500M FINAL
POS
NAME
REGION
TIME
1.
AMINA MOHAMED MGOHO
ARUSHA
4:38.59
2.
DORCAS BONIFACE ILANDA
PWANI
4:40.19
3.
ESTER MARTIN
SINGIDA
4:41.88
4.
FAIZA ALLY
SINGIDA
4:43.65
5.
CECILIA GINOKA
ARUSHA
4:44.22
6.
ANASTAZIA DOLOMONGO
ARUSHA
4:49.05
7.
OLIVA FRANCIS NADE
MANYARA
4:50.89
8.
ASHA MZUMARI
MARA
4:57.64
9.
ROSEMARY GUSTAPH
KUSINI UNGUJA
5:00.03
10.
ZAYANA MBEDULE
IRINGA
5:01.19
11.
YUSTA NINGA
MANYARA
5:02.12
12.
ANASTAZIA MKAMA
MARA
5:02.59
13.
ZAKIA SAID
SINGIDA
5:11.39
14.
FROLA JOHN
GEITA
5:11.84
15.
ESTER BWIRE
MARA
5:18.14
16.
EVELINA ERICK
TABORA
5:19.22
17.
RETICIA KIDILA
SIMIYU
5:21.31
18.
MARIAM LINGWA
GEITA
5:23.36
19.
RENATH YUSTUS
KAGERA
6:31.34

5000M FINAL
POS
NAME
REGION
TIME
1.
NATALIA  ELISANTE
ARUSHA
16:49.87
2.
CECILIA GINOKA
ARUSHA
16:55.36
3.
AMINA MGOHO
ARUSHA
17:07.60
4.
ANGELINA JOHN
SINGIDA
17:34.03
5.
ANASTAZIA MKAMA
MARA
17:56.32
6.
NOELA REMI
MANYARA
17:59.28
7.
KATALINA PHILI
MANYARA
18:48.93
8.
VIOLETH ADAM KILAS
NJOMBE
19:34.68
9.
EVELINA ERICK
TABORA
20:40.13
10.
DIANA BUKADI
KAGERA
20:40.13
11.
SUZANA MODEST
SIMIYU
20:47.38
12.
AMINA TINDI
TANGA
21:07.10
13.
SALIDA MANONGA
DSM
21:30.31
14.
NYENDO MTUMWA
KATAVI

15.
VERO MUMBA
NJOMBE

16.
OLIVIA EMANUEL
KAGERA



10,000M
POS
NAME
REGION
TIME
1.
NATALIA ELISANTE
ARUSHA
35:49.45
2.
ANGELINA JOHN
ARUSHA
37:18.55
3.
ROZALIA FABIAN
ARUSHA
37:27.84
4.
NOEL REMI
MANYARA
39:23.68
5.
CATHERINA MARGWE
MANYARA
39:28.91
6.
VIOLETH ADAMU
NJOMBE
42:20.40
7.
SUZANE MODEST
SIMIYU
44:25.31
8.
NEEMA ANDREW
KAGERA
48:02.63
9.
NYENDO MTUNDU
KATAVI
48:48.21

JAVELIN
POS
NAME
REGION
DISTANCE
1.
TAMA JAHA
MJINI MAGHARIBI
34M.48CM
2.
JOYCE BARNABAS
DODOMA
33M.73CM
3.
ANNET MICHAEL
DAR ES SALAAM
31M.39CM
4.
MAGDALENA TEMBO
MANYARA
28M.55CM
5.
VERONICA PAUL
DAR ES SALAAM
28M.09CM
6.
MERY EMILY
DAR ES SALAAM
24M.57CM
7.
NYAMIZI MATETED
TABORA
24M.37CM
8.
DIANA RAFAEL
IRINGA
23M.69CM



OVER ALL WINNERS

S/N
JINA LA MKOA
GOLD
SILVER
BRONZE
1.
ARUSHA
3
2
3
2.
DODOMA
-
1
-
3.
DAR ES SALAAM
-
1
2
4.
GEITA
-
-
-
5.
IRINGA
-
-
-
6.
KAGERA
-
-
-
7.
KASKAZINI PEMBA
-
-
-
8.
KASKAZINI UNGUNJA
-
-
-
9.
KATAVI
-
-
-
10.
KILIMANJARO
-
-
-
11.
KUSINI PEMBA
-
-
-
12.
KUSINI UNGUJA
2
1
1
13.
LINDI
-
-
-
14.
MANYARA
-
-
-
15.
MARA
-
-
-
16.
MBEYA
-
-
-
17.
MJINI MAGHARIBI
2
-
-
18.
MOROGORO
-
-
-
19.
MTWARA
-
-
-
20.
MWANZA
-
-
-
21.
NJOMBE
-
-
-
22.
PWANI
1
2
2
23.
RUVUMA
-
-
-
24.
SHINYANGA
-
-
-
25.
SIMIYU
-
-
-
26.
SINGIDA
-
1
-
27.
SONGWE
-
-
-
28.
TABORA
-
-
-
29.
TANGA
-
-
-