Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akiangalia baadhi ya mikataba iliyoingiwa na shirika hilo.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (MB) leo tarehe 17 Aprili, 2018 amefanya ziara ya
kushtukiza Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania.
Mhe. Profesa
Mbarawa ametembelea Makao Makuu ya
Shirika la Posta Tanzania kwa lengo la kukagua utendaji na uendeshaji wa
shughuli mbalimbali za Posta, katika ziara hiyo Mhe. Waziri aliongozana na
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Posta Luteni Kanali mstaafu Dr.
Haruni Kondo.
Katika ziara hiyo Waziri alitaka kujionea matumizi ya mifumo ya kielektronik na namna
ambavyo Shirika limejipanga kuitumia mifumo mbalimbali ili kusimamia utendaji
kwa ukaribu.
Mhe. Waziri
Mbarawa alitembelea idara ya Fedha, Idara ya Barua na Logistiki, Idara ya
Sheria, Idara ya Masoko na pia alikagua mifumo
udhibiti wa gharama za mafuta na mwenendo wa magari ya Shirika
yanayosafiri kati ya Dar es Salaam na
mikoani.
Katika ziara hiyo
Mh. Waziri ameitaka menejimenti ya Shirika kusimamia utendaji kazi na
kuzingatia weledi na matumizi ya mifumo ya kielektroniki na kufanya kazi kwa
bidii kwa kuzingatia kasi ya Serikali ya awamu ya tano na kuacha kufanya kazi
kwa mazoea.
Mhe. Waziri
alitoa msisitizo wa kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi na kukuza tija
kwa kila Idara ndani ya Shirka la Posta. Waziri amemwaagiza Kaimu Postamasta
Mkuu Hassan Mwang’ombe kufuatilia utendaji wa kila idara na kupata taarifa za
mara kwa mara ili kuimarisha utendaji wa shirika.
Mwenyekiti wa
Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Posta alimshukuru Waziri Mhe. Mbarawa kwa
kutembelea Shirika la Posta na kuahidi kuwa maagizo yote na maelekezo
aliyoyatoa atayasimamia kikamilifu ili kuleta tija na Ufanisi zaidi.
No comments:
Post a Comment