ALGIERS, Algeria
WATU 257 wamekufa
baada ya ndege ya jeshi kuanguka Kaskazini ya Algeria, wizara ya ulinzi inasema.
Tukio hilo limetokea
muda mfupi baada ya ndege kuondoka kutoka katika kiwanja cha ndege cha jeshi
cha Boufarik kilichopo jirani na mji mkuu wa Algiers asubuhi.
Wengi waliokufa ni
askari na familia zao, kwa mujibu wa wizara ya ulinzi. Wafanyakazi 10 wa ndege
hiyo nao waliuawa katika ajali hiyo.
Hatahivyo, bado
haijawekwa wazi kilichosababisha ajali hiyo.
Kiongozi wa jeshi
ameamuru kufanyika kwa uchukuzi ili kujua chanzo cha ajali hiyo, na aliahidi
kutembelea eneo la tukio.
Ndege nyigine
iliyoua watu wengi tangu Julai mwaka 2014,ilitokwa wakati watu 298 waliokuwa ndani ya ndege ya Malaysia
Airlines namba MH17 walipokufa wakati ilipotunguliwa mashariki ya Ukraine.
Hiyo ilikuwa ajali
ya pili kuuawa watu wengi katika ajali ya ndege tangu mwaka 2003.
Mamlaka zinafanyia kazi
kutambua mahiti ya waliokufa katika
ajali hiyo. Picha za video kutoka eneo la tukio linaonesha moshi ukitoka katika
mabaki ya ndege hiyo.
Ndege hiyo aina ya Ilyushin
Il-76, ilikuwa ikisafiri kutoka Bechar kusini-magharibi ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment