Waziri wa Uchukuzi na Mawasiano, Makame Mbarawa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) jijini Dar es Salaam leo. |
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
inatarajia kukusanya kiasi cha Sh bilioni 134 kupitia viwanja vyake kwa mwaka
wa fedha 2018-19, imeelezwa.
Pia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Richard Mayongela amesema
leo kuwa mamlaka yake iko mbioni kuanzisha tozo mpya ya usalama, ambayo huko
nyuma haikuwepo na inatarajia kuwaongezea mapato.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Rochard Mayongela akizungumza baada ya uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa TAA. |
Mayongela alisema kuwa Waziri wa Mawasiliano na
Uchukizi, Profesa Makame Mbarawa ameridhia kuanzishwa kwa tozo hiyo ya usalama,
ambayo watatozwa abiria wanaondoka kupitia viwanja vya ndege hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo na Mayongela, ambaye ni mwenyekiti
wa baraza hilo la wafanyakazi la TAA, ambalo ni la 21 wakati likizinduliwa leo katika
jengo la NSSF Ilala Jijini Dar es Salaam.
Anasema Waziri ameridhia kuanzishwa kwa tozo hiyo ya
usalama kutokana na changamoto zilizopo za kiusalama katika viwanja vyetu vya
ndege.
Alimshukuru Waziri kwa kufika licha ya majukumu mengi
aliyonayo katika kpindi hiki cha Bunge la Bajeti kinachoendelea mjini Dodoma, ambapo
alisema kuwa wafanyakazi wanataka kusikia maslahi yao yanaboreshwa.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakati wa uzinduzi wa baraza hilo leo. |
Mbarawa aliwapongeza wafanyaakzi wote waliochaguliwa
kuwa wajumbe wa baraza hilo na kuwaambia kuwa kazi ndio kwanza inaanza na wao
ndio injini na ndio wanaangalia maslahi ya wafanyakazi, kwani wao ndio kiungo
kati ya wafanyakazi na uongozi.
Alisema Serikali inawathamini sana na wako pale
kisheria na aliwataka kushirikiana na serikali, ambapo pia aliwakumbusha
majukumu yao baada ya kuchaguliwa.
Alitaka wajumbe wa baraza hilo kujiuliza
wamewafanyoia nini wadau wa viwanja vya ndege na wamewafanyia nini Watanzania
na kupanga bajeti vizuri na kama hawajafikia amewataka kuhoji sababu za
kutofikia bajeji ya mwaka 2017-18 na kama wamefikia malengo wajipongeze.
Pia amewataka kujiuliza sababu za viwanja vya ndege
Tanzania Bara kutokuwemo katika orodha ya viwanja 10 bora vya ndege barani
Afrika, wakati Zanzibar kimo katika viwanja bora.
Alihoji sababu za TAA kushindwa hata kununua gari la
zima moto na badala yake kusubiri fedha kutoka Serikali Kuu wakati wana vyanzo
vingi vya mapato, ambavyo kama wangevitumia vizuri wangeweza kujinuliwa wenywe
magari hayo.
Alisema Watanzania na wasafiri wengi bado wana imani
na viwanja vya ndege vya Tanzania, lakini tatizo ni kasoro ndogo ndogo ndizo
zinafanya tushindwe kuwa miongoni mwa viwanja bora barani Afrika.
Alisema kama hatuko katika viwanja bora huo ndio mwanzo
wa kupoteza watalii kwani wengi watakimbilia Kenya ambako kuna viwanja bora
kuliko sisi na wakipungua, basi wafanyakazi wengine watapunguzwa.
Aliwataka kufanyakazi kwa bidii ili kujiongezea
mapato na kubuni miradi mingine, ambayo itawawezesha kupata fedha, na
alimpngeza Mayongela kwa kuwa nampango wa kununia magari sita kwa mpigo, kitu
ambacho huko nyuma hakijawahi kufanywa.
No comments:
Post a Comment