Failuna Abdi (kulia) aliyeshindwa kupata medali katika mbio za meta 10,000 katika Michezo ya Madola. Kushoto ni Jackline Sakilu. |
Na Mwandishi Wetu
MATUMAINI ya Tanzania ya kupata medali katika Michezo
ya 21 ya Jumuiya ya Madola inayoendelea Gold Coast, Australia, yanazidi kufifia
baada ya mwanariadha mwingine, Failuna Abdul kumaliza katika nafasi ya 12
katika mbio za meta 10,000.
Tayari mwanariadha mwingine wa Tamzania, Ali Rashid
Gulam kumaliza wan ne katika kundi lake la mchujo na kushindwa kufuzu hatua
inayofuata katika mbio za meta 100 zilizofanyika juzi mjini humo.
Failuna alimaliza mbio hizo za meta 10,000 kwa
kutumia dakika 32:22.01 ikiwa ni sekunde 37 nyuma ya mshindi wa kwanza Stella
Chegan wa Uganda aliyemaliza wa kwanza kwa kutumia dakika 31:45.03 akifuatiwa
na Mkenya, Stacy Ndiwa aliyemaliza kwa muda wa 31:46.04.
Mshindi watatu aliyepata medali ya shaba ni Mercline
Chelangat wa Uganda aliyetumia dakika 31:48.04.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT),
Wilhelm Gidabuday alisema jana kuwa, Failuna amejitahidi sana kwa kupishana na
mshindi wa kwanza kwa sekunde 37 tu, ambapo alisisitiza kuwa mbio hizo zilikuwa
za ushindani mkubwa.
Gidabuday amesema kuwa wanasubiri mbio za meta 5,000
ambazo atashiriki tena Failuna huku tegemeo lao kubwa liibaki kwa Said Makula
na Sarah Ramadhani ambaowatashiriki marathon pamoja na Stephano Huche siku ya
mwisho ya michezo hiyo, Aprili 15.
No comments:
Post a Comment