Na Mwandishi Wetu
VINARA wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, Simba wanazidu kuukaribia ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bada, baada ya kuifunga Mbeya City kwa mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 55 ikifunga mabao 55 katika michezo 23, ikifuatiwa na mahasimu wao, Yanga waliopo katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 47 katika michezo 22 na nafasi ya tatu Azam yenye pointi 45 katika michezo 23.
Mabao ya Simba yalifungwa na Emmanuel Okwi, John
Bocco na Asante Kwasi, huku lile la kufutia machozi la Mbeya City likiwekwa kimiani na Frank Ikobela.
Simba ilianza kwa kasi mchezo huo na kupata bao la
uongozi dakika ya 16 lililofungwa na Okwi, likitokana na shuti la Bocco lililopanguliwa na kipa wa City, Owen
Chaima kuzagaa eneo la hatari.
Dakika 29 Bocco alipata nafasi ya wazi na kushindwa
kuitumia baada ya kupiga mpira pembeni ya goli lakini dakika 32 baadaye Kwasi
akaifungia Simba bao la pili kwa kichwa akipata krosi ya Shiza Kichuya.
Kabla ya wekundu hao kufunga bao la tatu dakika 35
lilifungwa na Bocco kutokana na krosi ya Shomari Kapombe, tayari City walifunga
bao dakika 34 lililotokana na kona iliyochongwa na Danny Joram na kmkuta Ikobelo
na kuujaza wavuni kwa kichwa.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Simba ilikuwa
mbele mabao 3-1 wakiongoza kwa kufanya mashambulizi mengi lakini pia, walitumia
faida ya wapinzani waliotumia muda mwingi kujilinda.
Kipindi cha pili Simba ilikuja na mbinu za kujihami
na kushambulia kiasi na wapinzani wao
walikuja kwa kasi wakitafuta nafasi ya kufunga lakini walishindwa kutumia nafasi
kadhaa walizopata. Dakika ya 65 Victor Hangaya nusura afunge kipa wa Simba
Manula aliudaka.
Pia, Simba nusura ifunge dakika ya 53 mpira uligonga
mwamba na dakika ya 57 Kichuya alipiga shuti kali golini lilipanguliwa na
Chaima.
Hadi dakika 90 zinamalizika hakuna aliyeongeza bao na
Simba ikiibuka na pointi tatu muhimu.
Michezo mingine iliyochezwa jana, Mtibwa imeshinda
bao 1-0 dhidi ya Ndanda huku mchezo wa Ruvu Shooting dhidi ya Azam ukiahirishwa
kutokana na mvua kubwa kunyesha Mlandizi.
Vikosi Simba;Aishi Manula, Nicholaus Gyan/James Kotei dk.87,
Asante Kwasi/Mohamed Hussein dk. 73, Juuko Murshid, Yusufu Mlipili, Erasto
Nyoni, Jonas Mkude, Shomari Kapombe, Emmanuel Okwi, John Bocco/Laudit Mavugo
dk. 79 na Shiza Kichuya.
Mbeya City:Owen Chaima, Rajabu Isihaka, Majaliwa
Shabani, Ally Lundenga, Ramadhan Malima, Haruna Shamte, Eliud Ambokile, Danny
Joram/Danny Joram dk. 60, Victor Hangaya/Godfrey Milla dk. 76, Babu Ally/Hamidu
Mohamed dk.43 na Frank Ikobela.
No comments:
Post a Comment