Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Singida United ambao Jumapili iliyopita
iliifunga Yanga kwa penalti 4-2 na kuitoa katika mashindano ya Kombe la
Shirikisho la Azam, jana walikiona cha moto baada ya kufungwa 3-0 na Mtibwa
Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar imefikisha pointi 30 na
kuendelea kuwa katika nafasi ya sita huku wanyonge Singida wawakibajki katika
nafasi ya tano na pointi zao 35.
Kelvin Sabato ndiye aliyekuwa wa kwanza kuifungia bao
Mtibwa katika katika dakika ya 22 katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja
wa Namfua mjini Singida.
Bao la pili la Mtibwa Sugar lilifungwa na Kihimbwa katika dakika ya 53 wakati la tatu, liliwekwa
kimiani na Hassan Dilunga kwa penalti katika dakika ya 71 baada ya mchezaji
mmoja wa Mtibwa kuchezewa vibaya katika eneo la hatari.
No comments:
Post a Comment