PARIS, Ufaransa
KLABU ya Paris St-Germain imetwaa taji la Ligi Kuu
ya Ufaransa ya Ligue 1 kiaina, baada ya kuwachapa mabingwa watetezi Monaco
kwa mabao 7-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Parc des Princes.
PSG inayomilikiwa na raia wa Qatar, imetwaa ubingwa
huo baada ya kuongoza kwa pointi 17 dhidi ya Monaco iliyopo katika nafasi ya
pili.
Giovani lo Celso na Angel di Maria wote walifunga
mabao mawili kila mmoja wakati Edinson Cavani na Julian Draxler nao pia
walifunga.
Radamel Falcao alikamilisha ushindi wa PSG wakati Rony
Lopes ndiye aliyefunga bao la kufutia machozi kwa Monaco katika mchezo huo
uliokuwa wa upande mmoja, ukitawaliwa na washindi.
Monaco ilitwaa taji lake la mara ya kwanza miaka 17
iliyopita katika msimu wa mwaka 2016-17.
Falcao anabaki na Monaco lakini Mbappe – ambaye
alijiunga na PSG kwa ada ya pauni milioni 166, awali kwa mkopo, na wachezaji
wengine muhimu kama beki Benjamin Mendy aliyeondoka katika klabu hiyo wakati wa
majira yaliyopita ya kiangazi.
PSG iliifunga Monaco 3-0 katika fainali ya Kombe la
Ligi la Ufaransa mwishoni mwa mwezi uliopita na kiwango chao kimeonekana
kuongezeka.
Beki Mbrail Dani Alves alitoa krosi kwa Muargentina Lo
Celso katika dakika ya 14 na kuifungia timu yake.
Mchezaji wa kimataifa wa Uruguay, Cavani aliongeza la
pili kwa shuti kali la kichwa akiunganisha krosi ya winga Mjerumani Draxler
kabla Di Maria hajafunga.
PSG ilimteua kocha wazamani wa Sevilla Unai Emery kama
kocha wao mpya kwa miaka miwili kuanzia Juni 2016 na msimu mmoja baadae
alitarajiwa tofauti na ilivyofikiriwa ametwaa taji.
Hatahivyo, PSG imesikitishwa na kutolewa katika
mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kutoka kwa Real Madrid na kuacha swali
kuhusu hatma yake.
Inatarajia kuwa Emery ataondoka klabuni hapo mwishoni
mwa msimu, huku kocha wazamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel ndiye
anayefikiriwa kubeba mikoba hiyo.
No comments:
Post a Comment